Pata taarifa kuu

Takribani watu 7,703 wafariki katika vita kati ya Israel na Hamas.

Wizara ya afya katika eneo la Hamas imesema kuwa takribani watu 7,703 wameuwawa katika vita na Israeli vilivyoanza tarehe 7 ,Octoba .Wizara hiyo vilevile imesema kuwa watoto 3,500 ni miongoni mwa waliofariki .

Kikosi cha kijeshi cha Israel kinaonekana kikiwa karibu na mpaka wa Israel na Gaza, Israel, Jumamosi, Oktoba 28, 2023.
Kikosi cha kijeshi cha Israel kinaonekana kikiwa karibu na mpaka wa Israel na Gaza, Israel, Jumamosi, Oktoba 28, 2023. AP - Ohad Zwigenberg
Matangazo ya kibiashara

Usiku wa kuamkia leo Israel ilifanya mashambulio ya mabomu usiku kucha kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Kulingana na taarifa ni kuwa ndege mia moja za kivita zilitumika katika shambulio hilo na kwa sasa wanajeshi wa Israel wamejikita katika eneo la kaskazini mwa ukanda wa Gaza, huko Beit Hanoun, na kuelekea upande wa kusini.

Kanda ya video iliyosambazwa kutoka Gaza asubuhi ya leo inaonyesha kile kilichotokea jana usiku katika eneo hilo, iikiashiria shambulio kubwa la bomu .

Wizara ya ulinzi ya Palestina pia imeongeza kuwa maelfu ya manyumba na mamia ya majengo yaliharibiwa.

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israeli Daniel Hagari aliambia vyombo vya habari kuwa vikosi vya Israel viliingia katika eneo la kaskazini mwa Ukanda wa Gaza na kufanya mashambulio ya ardhini, angani na baharini na kwamba makamanda wa Hamas waliuawa .

Israel inasema inalenga mtandao wa mahandaki ambao kundi hilo limejenga chini ya ardhi huku likianzisha mashambulio ya anga mjini Gaza kujibu mashambulio ya Hamas kusini mwa Israel.

Hata hivyo viongozi kutoka Mataifa mbalimbali pamoja na umoja wa mtaifa  wametoa wito kwa pande kinzani katika mzozo wa Israel ana Palestina kusitisha makabiliano makali yaliyozuka tarehe 7 mwezi Oktoba , wakati wapinganaji wa Palestina Hamas walipoanzisha mashambulkio ya kushtukiza dhidi ya Israel

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.