Pata taarifa kuu

Mamia kwa maelfu waandamana London kwa mshikamano na wakaazi wa ukanda wa Gaza

Maandamano ya kuwaunga mkono Wapalestina yamepamba moto katika mitaa ya London huku yale yaliyokuwa yafanyike Paris yamepigwa marufuku na Mahakama ya Utawala; kwa sababu ya "hatari ya kuyumbishwa kwa usalama wa taifa". hata hivyo shirika lisilo la kiserikali la Amnesty International limelaani marufu hiyo na kusema, "hiki ni kikwazo kipya kwa haki ya kuandamana".

Katika mji mkuu wa Uingereza mnamo Oktoba 28, 2023.
Katika mji mkuu wa Uingereza mnamo Oktoba 28, 2023. REUTERS - SUSANNAH IRELAND
Matangazo ya kibiashara

Ni umati tulivu unaoandamana kwa amani kando ya kingo za Mto Thames, anasema mwandishi wetu wa London, Marie Boeda. Helikopta inasikika kwa mbali na waandamanaji wakipeperusha bendera za Palestina. Kwenye mabango wanayoshikilia yanaandikwa: "Sitisheni mapigano mara moja", "Acheni kulipua Gaza", "Msifadhili mauaji ya kimbari". Kuna vijana wengi na wengi pia wanasema kwamba wanakuja kwa mara ya kwanza leo, kwa sababu ya kile kilichotokea usiku wa jana huko Gaza. Mkaazi wa London mwenye umri wa miaka 22 ameniambia kwamba sasa aliona kuwa ni wajibu wake kuoandamana. Zaidi ya maafisa wa polisi elfu moja wametumwa leo kusimamia maandamano haya, na tofauti na wiki iliyopita, wakati huu, ikiwa baadhi ya waandamanaji wataimba "jihad", polisi wana jukumu la kuingilia kati. Vivyo hivyo kwa wale wanaoshikiliamabango kuunga mkono Hamas. Kwa sasa, hatuoni yoyote. Huko Uingereza, maandamano kwa ujumla ni tulivu.

London, Jumamosi Oktoba 28, 2023.
London, Jumamosi Oktoba 28, 2023. REUTERS - SUSANNAH IRELAND

Wizara ya Afya ya Hamas imetangaza kwamba watu 7,703 wameuawa katika Ukanda wa Gaza tangu kuanza kwa vita na Israel. Kulingana na wizara hiyo, zaidi ya watoto 3,500 ni miongoni mwa vifo vilivyorekodiwa tangu kuanza kwa vita Oktoba 7. Ripoti ya hivi punde iliyowasilishwa Ijumaa ilibainisha vifo 7,326.

Wakati huo huo ndege isiyo na rubani ya jeshi la Israel imeshambulia kundi la wapiganaji wa Hezbollah waliokuwa wakijaribu kurusha makombora kutoka Lebanon kuelekea Israel siku ya Jumamosi, msemaji wa jeshi la Israel amesema, akinukuliwa na Gazeti la kila siku la Haaretz.

Hayo yakijiri afisa mkuu wa Hamas, Moussa Abou Marzouk, anayezuru Moscow, amesema kuwa kuldi la Hamas linajaribu kubainisha eneo la mateka wanane wenye uraia wa Urusi na Israel ili kuwaachilia. "Sasa tunatafuta watu ambao waliripotiwa na upande wa Urusi. Ni ngumu, lakini tunatafuta. Na mara tu tutakapowapata, tutawaachia,” afisa huyo amesema, akinukuliwa na shirika la habari la serikali ya Urusi Ria Novosti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.