Pata taarifa kuu

Washington na washirika wake 'wapinga vikali' hatua ya Israel ya kupanua makaazi ya walowezi

Washington, Berlin, Paris, Rome na London zimesema "zinapinga vikali", uamuzi wa Israeli wa kuhalalisha makazi tisa katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa na mradi wa makazi mapya katika makazi yaliyopo, ambayo ni 'kuongeza tu mvutano' kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Wanajeshi wa Israel wanamkamata mmoja wa waandamanaji wanaoandamana dhidi ya makazi ya Wayahudi karibu na Ramallah mnamo Desemba 6.
Wanajeshi wa Israel wanamkamata mmoja wa waandamanaji wanaoandamana dhidi ya makazi ya Wayahudi karibu na Ramallah mnamo Desemba 6. REUTERS/Mohamad Torokman
Matangazo ya kibiashara

"Tunapinga vikali vitendo hivi vya upande mmoja ambavyo vinaongeza tu mvutano kati ya Waisraeli na Wapalestina na ambavyo vinadhoofisha juhudi za kufikia suluhisho la nchi mbili lililojadiliwa," wameandika wakuu wa diplomasia wa nchi hizo tano, katika taarifa ya pamoja, shirika la habari la AFP limeripoti.

Mawaziri hao wamesema wataendelea kufuatilia hali ilivyo. Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken, jana Jumatatu alikosoa mpango wa Israel wa kuendelea na ujenzi huo. 

Zaidi ya Waisraeli 475,000 wanaishi katika makaazi ya walowezi katika Ukingo wa Magharibi wanakoishi pia Wapalestina milioni 2.8.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.