Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Ramallah: Antony Blinken aelezea 'huzuni' yake baada ya vifo vya 'Wapalestina wasio na hatia'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ameelezea "huzuni" yake baada ya vifo vya "Wapalestina wasio na hatia" katika ghasia za Waisrael na Wapalestina, katika mkutano na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa kwa mabavu. Antony Blinken ametoa wito wa 'kukomeshwa kwa uhasama'.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) akutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Ramallah, Jumanne, Januari 31, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken (kushoto) akutana na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas katika mji wa Ukingo wa Magharibi wa Ramallah, Jumanne, Januari 31, 2023. AP - Majdi Mohammed
Matangazo ya kibiashara

"Niruhusuni nianze kwa kuwasilisha rambirambi zangu na kuelezea masikitiko yangu kwa vifo vya raia wasio na hatia wa Palestina ambao wamepoteza maisha katika ghasia katika mwaka uliopita," Antony Blinken amesema kwenye makao makuu ya Mamlaka ya Palestina huko Ramallah, uko Ukingo wa Magharibi, katika eneo la Palestina linalokaliwa na Israel tangu mwaka 1967.

Ghasia za Israel na Palestina ziligharimu maisha ya watu 235 mwaka 2022, karibu asilimia 90 ya Wapalestina, kulingana na hesabu za shirika la habari la AFP zilizokusanywa kutoka kwa vyanzo rasmi vya Israeli na Palestina. Kulingana na Umoja wa Mataifa, mwaka uliopita umekuwa mbaya zaidi tangu 2005 katika Ukingo wa Magharibi.

Israel katika visa vingine imekiri kwamba vikosi vyake viliwaua raia kimakosa katika uvamizi uliowasilishwa kama "kukabiliana na ugaidi".

"Wapalestina, kama Waisraeli, wana hisia zinazoongezeka za ukosefu wa usalama, hofu inayoongezeka nyumbani, katika jamii zao na katika maeneo yao ya ibada," Antony Blinken amesikitika huko Ramallah.

"Tunafikiri ni muhimu kuchukua hatua za kutokomeza machafuko haya, kukomesha ghasia, kupunguza mivutano (...)", ameongeza, akionya dhidi ya hatua yoyote ambayo inahatarisha suluhu kwa mataifa mawili, Israel na Palestina.

  Alitaja "upanuzi (wa Israeli) wa makazi, kuhalalisha vituo vya nje (visivyoidhinishwa na serikali), ubomoaji wa nyumba na kufukuzwa kwa Wapalestina" kama sera za serikali ya Israeli.

Bw. Blinken pia amelaumu “kufifia kwa upeo wa matumaini kwa Wapalestina. Hili pia, tunaamini, lazima libadilike.”

Baadhi ya Waisraeli 475,000 wanaishi katika makazi ya Wayahudi - kinyume cha sheria chini ya sheria za kimataifa - katika Ukingo wa Magharibi, ambapo karibu Wapalestina milioni 2.9 wanaishi.

Ziara ya mkuu wa diplomasia ya Marekani, ambayo ilipangwa kwa muda mrefu, ilianza Jumapili nchini Misri na kumalizika Jumanne jioni. Inatokea baada ya siku kadhaa za ghasia zilizoambatana na mashambulizi ya Wapalestina huko Jerusalem Mashariki ambayo yalisababisha vifo saba na uvamizi mbaya wa jeshi la Israel katika Ukingo wa Magharibi.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.