Pata taarifa kuu

Antony Blinken atoa wito kwa Waisraeli na Wapalestina 'kutochochea mvutano'

Akitokea Cairo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken amewasili Jumatatu, Januari 30, nchini Israel na Palestina ili kujaribu kushawishi pande hizo mbili kupunguza hali ya wasiwasi katika eneo hilo. Ziara ambayo inaoneka kuwa ngumu. Antony Blinken ametoa wito kwa Waisraeli na Wapalestina 'kutochochea mvutano'.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion nchini Israel, karibu na Tel Aviv, Jumatatu, Januari 30, 2023.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitoa hotuba alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion nchini Israel, karibu na Tel Aviv, Jumatatu, Januari 30, 2023. AP - Ronaldo Schemidt
Matangazo ya kibiashara

"Ni jukumu la kila mtu kuchukua hatua za kupunguza mvutano badala ya kuuchochea..." amesema alipowasili Tel Aviv. "Ndiyo njia pekee ya kumaliza wimbi la ghasia ambalo limegharimu maisha ya watu wengi: maisha ya Waisraeli wengi, maisha ya Wapalestina wengi. "

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani anatarajia kuzuru Jerusalem na Ramallah. Ziara iliopangwa kwa muda mrefu, lakini ambayo inakuja wakati kunaripotiwa kuzorota kwa hali ya usalama, anaripoti mwandishi wetu huko Jerusalem, Michel Paul.

Antony Blinken atawataka viongozi wa nchi hizi mbili, Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas na Waziri Mkuu wa Israel Binyamin Netanyahu, kuchukua hatua za haraka za kupunguza hali hiyo.

Siku ya Jumanne Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani atakutaka kwa mazungumzo na Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina Mahmoud Abbas. Antony Blinken anataka kumshawishi Mahmoud Abbas kudumisha mazungumzo na Waisraeli.

Kufuatia shambulio la mauaji lililofanywa na jeshi la Israel huko Jenin, mamlaka ya Palestina ilitangaza kuwa itasimamisha uratibu wa usalama na Israel. Uamuzi wa kusikitisha, Washington imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.