Pata taarifa kuu

Israel kupanua operesheni zake za ardhini huko Gaza

Mashambulio makali ya Israel yanaendelea Ijumaa jioni, Oktoba 27, katika Ukanda wa Gaza, ambapo Umoja wa Mataifa, ambao unatoa wito wa kusitishwa kwa mapigano, unahofia "mateso yasiyo na kifani kwa raia wa gaza wasio kuwa na hatia."

Picha hii iliyopigwa kutoka kwa video ya televisheni ya AFP inaonyesha moto na moshi ukifumba juu ya Jiji la Gaza wakati wa shambulio la Israeli, Oktoba 27, 2023.
Picha hii iliyopigwa kutoka kwa video ya televisheni ya AFP inaonyesha moto na moshi ukifumba juu ya Jiji la Gaza wakati wa shambulio la Israeli, Oktoba 27, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake kwa njia ya televisheni, msemaji wa jeshi la Israel pia ametangaza kwamba wanapania "kupanua operesheni zao za ardhini jioni hii" huko Gaza, huku Hamas ikitoa wito kwa jamii ya kimataifa "kuchukua hatua mara moja" kukomesha mashambulizi ya Israel.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio linalotaka "kusitisha mapigano" kati ya Hamas na Israel kwa ajili ya kupitisha misaada. Azimio hilo lisilo la kisheria, lililolaaniwa na Israel na Marekani ambao wameshutumu kutotajwa kwa Hamas, limepata kura 120 na kupigiwa makofi, dhidi ya 14 zilizopinga, na wajumbe 45 wamejizuia kutoa msimamo wao, kati ya wanachama 193 wa Umoja wa Mataifa.

Kwa saa kadhaa tumekuwa tukishuhudia kuongezeka kwa mashambulizi ya anga kwenye Ukanda wa Gaza, anakumbusha mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul. 

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF), Daniel Hagari anasema Hamas "inaendesha vita kutoka kwa hospitali" huko Gaza kwa kutumia vifaa hivi kama "miundombinu ya ugaidi".

Anaashiria hospitali ya Al Shifa, ambayo ni kubwa zaidi katika Ukanda wa Gaza.

Pia ameelezea mtandao wa kina wa vichuguu chini ya jengo katika Jiji la Gaza, ambapo anasema mashambulizi yanaweza kupangwa.

Hagari anasema "mamia ya magaidi walikimbilia hospitali kujificha humo" baada ya mashambulizi dhidi ya Israel tarehe 7 Oktoba, na anasema Israel ina taarifa za kijasusi kwamba "kuna mafuta katika hospitali za Gaza, na Hamas inayatumia kwa miundombinu yake ya ugaidi".

Kwa upande wake Hamas imekana madai ya jeshi la Israel - kwamba limekuwa likitumia hospitali katika Ukanda wa Gaza kama kambi ya kuendeleza vita.

Mjumbe wa ofisi ya kisiasa ya kundi hilo amenukuliwa na shirika la habari la Reuters akisema kuwa Israel ilitoa madai hayo kama "utangulizi wa kufanya mauaji mapya dhidi ya watu wetu".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.