Pata taarifa kuu

Misaada ya kibinadamu inaweza kuanza kuwasili Gaza kuanzia Ijumaa

Misaada ya kibinadamu inapaswa kuanza kuingia Gaza Ijumaa Oktoba 20, kulingana na habari iliyotolewa Alhamisi hii na idhaa ya Misri ya AlQahera News. Huko Rafah, magari makubwa ya mizigo yaliyosheheni misaada yako tayari kusaidia Wagaza. Shirika la Afya duniani linabaini kwamba "janga la kibinadamu" linatishia wakaazi wa Gaza.

Malori ya misaada ya kibinadamu bado yanasubiri karibu na kivuko cha mpaka cha Rafah upande wa Misri mnamo Oktoba 19, 2023. Yanapaswa kuingia Gaza kuanzia Oktoba 20.
Malori ya misaada ya kibinadamu bado yanasubiri karibu na kivuko cha mpaka cha Rafah upande wa Misri mnamo Oktoba 19, 2023. Yanapaswa kuingia Gaza kuanzia Oktoba 20. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Malori ya kwanza ya misaada ya kibinadamu kwenda Gaza, yaliyoahidiwa Jumatano na Misri na Marekani, yanaweza kuruhusiwa kupita kwenye kivuko cha mpaka cha Rafah siku ya Ijumaa Oktoba 20. Vyovyote vile, hivi ndivyo vyombo vya habari vilivyo karibu na ujasusi wa Misri vimetangaza Alhamisi hii. Kwa mujibu wa kituo cha Habari cha AlQahera, kituo cha Rafah kitafunguliwa siku ya Ijumaa ili kusafirisha misaada ya kibinadamu hadi katika ardhi ya Palestina.

Kwa mujibu wa gazeti la New York Times, likiwanukuu maafisa wa Umoja wa Mataifa (UN), makubaliano hayo yanasema bendera ya Umoja wa Mataifa itapandishwa wakati lori hizi zikipita na waangalizi wa kimataifa waweze kuzikagua kabla ya kuingia Gaza. Hili ni ombi kutoka kwa Israel, ambayo inahofia kwamba Hamas itachukua fursa hii kusafirisha silaha.

Ishara kwamba mambo yanaweza kubadilika: katika kituo cha Rafah, wafanyakazi wamefanya ukarabati wa miundombinu iliyokumbwa na mashambulizi hivi majuzi, ambapo karibu na malori kadhaa yameegeshwa. Hakuna maelezo yaliyotolewa kuhusu ni magari mangapi ya mizigo yantaruhusiwa kupita. Rais wa Marekani Joe Biden alitangaza aliambiwa na mwenzake wa Misri, Abdel Fatah al-Sissi, "kuruhusu hadi lori 20 zivuke".

Idadi haitoshi kabisa kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO). Mkuu wa shirika hili la Umoja aw Mataifa, Tedros Adhanom Ghebreyesus, pia amebaini kwamba hakuna uhakika kwamba msaada utaweza kuingia katika eneo hilo siku ya Ijumaa. WHO pia inatoa wito kwa Israeli kuruhusu usambazaji wa mafuta hadi Gaza, kwa jenereta za hospitali.

Antonio Guterres: "Tunahitaji juhudi za kudumu"

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesihi mjini Cairo siku ya Alhamisi kwa "ufikiaji wa haraka na usiozuiliwa wa kibinadamu" kwa ajili ya misaada ya kibinadamu kwa Gaza. Ametoa wito wa "kusitishwa mara moja kwa mapigano kwa ajili ya kupitisha misaada ya kibinadamu" katika siku ya 13 ya mapigano kati ya Israel na Hamas.

"Sheria ya kimataifa ya kibinadamu lazima iheshimiwe," amesisitiza Antonio Guterres wakati wa mkutano na waandishi wa habari na mkuu wa diplomasia ya Misri, Sameh Choukri. "Tunahitaji chakula, maji, mafuta na dawa mara moja, tunahitaji mengi na tunayahitaji shughuli hizi zuiendelee," ameongeza.

Antonio Guterres anasisitiza: “Kinachohitajika si operesheni ndogo bali ni juhudi za kudumu (...), mashirika ya kutoa misaada wanaombwa kuweza kuleta misaada na kuisambaza kwa usalama. (...) Ulinzi wa raia ni wa msingi, mashambulizi dhidi ya hospitali, shule au miundombinu ya Umoja wa Mataifa yanakwenda kinyume na sheria za kimataifa. "

Hatimaye, kiongozi wa Ureno alikuwa na maneno kuhusu wale wanaoshikiliwa mateka: "Hamas lazima iwaachilie mateka bila masharti na Israeli lazima ihakikishe upatikanaji wa haraka na bila vikwazo vya misaada ya kibinadamu kwa Wapalestina. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.