Pata taarifa kuu

Israel-Hamas: UNSC yakataa azimio la Urusi, mkutano mwingine Jumanne

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatatu jioni lilikataa azimio lililopendekezwa na Urusi la "kusitisha mapigano kati ya Israel na Hamas kwa ajili ya kupitisha na kutoa misaada ya kibinadamu", wakati Joe Biden anatarajiwa nchini Israel siku ya Jumatano.

Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York.
Moja ya vikao vya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, New York. ©REUTERS/Shannon Stapleton
Matangazo ya kibiashara

Wakati diplomasia inajitahidi kuepusha "janga la kibinadamu" na mzozo wa kikanda - vita tayari vimesababisha angalau vifo 1,400 kwa upande wa Israeli na 2,750 kwa upande wa Palestina - Baraza la Usalama litakutana Jumanne jioni kuamua juu ya rasimu ya azimio la pili lilowasilishwa na Brazil.

Rasimu ya azimio la Urusi iliidhinishwa na nchi tano wanachama wa Baraza - ikiwa ni pamoja na Urusi na China -, na kukataliwa na nchi zingine nne (Marekani, Uingereza, Ufaransa na Japan) na sita zilijizuia, pamoja na Brasil.

Ili kupitishwa, azimio linahitaji idhini ya angalau wanachama tisa kati ya 15 wa Baraza, bila kura ya turufu kutoka kwa mmoja wa wanachama watano wa kudumu (Marekani, Uingereza, Ufaransa, Urusi, China).

Balozi wa Urusi katika Umoja wa Mataifa Vasily Nebenzia alisikitika kwamba nchi za Magharibi "zimezuia ujumbe wa kawaida na wa kipekee kutoka kwa Baraza la Usalama kujibu masilahi ya ubinafsi na kisiasa."

Moscow "ina wasiwasi mkubwa juu ya janga la kibinadamu ambalo halijawahi kutokea huko Gaza na hatari kubwa ya mzozo kuenea" katika eneo zima, alionya mwanadiplomasia wa Urusi.

Mwenzake wa Uingereza Barbara Woodward amejibu kwamba London "haiwezi kuunga mkono azimio ambalo linaepuka kulaani mashambulizi ya kigaidi ya Hamas".

- 'Maisha ya Wapalestina' ni muhimu -

Akialikwa kuzungumza, Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa Riyad Mansour "amesikitika" kuona Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linashindwa "kuonyesha hata ishara kwamba maisha ya Wapalestina ni muhimu".

"Msithubutu kusema kuwa Israel haihusiki na mabomu inayorusha kwa maksudi na kuua Wapalestina, msihalalishe mauaji hayo (...) Kinachotokea Gaza sio operesheni ya kijeshi. Hii ni chokochoko ya kiwango cha juu dhidi ya raia wetu, mauaji dhidi ya raia wasio na hatia," mwanadiplomasia huyo wa Palestina amesema.

Balozi wa Israel Gilad Erdan, pia amealikwa, huku akikumbusha kwamba Umoja wa Mataifa ni"taasisi iliyoanzishwa (mwaka 1945) juu ya majivu ya Holocaust, mauaji ya kimbari ya watu wa Kiyahudi" na kwamba shambulio la mauaji la Oktoba 7 lililotekekezwa na Hamas, ambalo aliinganisha na “Wanazi,” lilikuwa “jaribio lingine la mauaji ya halaiki ya Wayahudi.”

Mkutano huo ulichukua muda wa saa tatu, huku Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akitangaza kutoka Tel Aviv kuhusu ziara ya rais Biden siku ya Jumatano kwa mshikamano na mshirika wake wa Israel.

Nchi 15 wanachama wa Baraza hilo pia zilipaswa kupigia kura azimio la pili lililowasilishwa na Brazil, mwenyekiti wa baraza hilo mwezi Oktoba.

Kulingana na wanadiplomasia, Baraza la Usalama litakutana tena Jumanne usiku w amanane saa za Afrika ya Kati.

Rasimu ya azimio la Urusi ilitaka "kusitishwa kwa mapigano mara moja, kudumu na kuheshimiwa kikamilifu" na ufikiaji "bila kuzuiliwa" wa misaada ya kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza ambayo inazingirwa na vikosi vya Israel.

Lakini bila ya kuitajwa Hamas, jambo ambalo Marekani, Uingereza na Ufaransa zimefutilia mbali.

Rasimu ya azimio la Brazil inalaani hasa "mashambulio ya kigaidi ya Hamas."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.