Pata taarifa kuu

Moja kwa moja: Mapigano makali yarindima Khan Younis inayozingirwa na Israel

Jeshi la Israel siku ya Jumatano limeuzingira mji mkubwa wa Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, ambapo baadhi ya mapigano makali zaidi katika miezi miwili ya vita dhidi ya Hamas yanapamba moto.

Wapalestina wanaoomboleza vifo vya ndugu zao waliouawa wakati wa milipuko ya mabomu ya Israeli katika hospitali ya Nasser huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 14, 2023.
Wapalestina wanaoomboleza vifo vya ndugu zao waliouawa wakati wa milipuko ya mabomu ya Israeli katika hospitali ya Nasser huko Khan Younes, kusini mwa Ukanda wa Gaza, Novemba 14, 2023. AP - Fatima Shbair
Matangazo ya kibiashara

Unachotakiwa kufahamu kuhusu vita vya Ukanda wa Gaza:

Jeshi la Israel siku ya Jumanne liliendeleza mashambulizi yake dhidi ya Hamas kusini mwa Ukanda wa Gaza ambako lilifanya mashambulizi mabaya. Vikosi vya arhini vimeingia katika jiji kubwa la Khan Younes na wanapigana vikali na wapiganaji wa Hamas, kulingana na mashahidi.

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA), hospitali ya Nasser huko Khan Younes, iliyozidiwa na wimbi la majeruhi na upungufu wa wafanyakazi na vifaa, inahudumia zaidi ya wagonjwa 1,000 na watu 17,000 waliokimbia makazi. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu milioni 1.8, karibu robo tatu ya watu, wamekimbia makazi yao kutokana na vita katika Ukanda wa Gaza.

"Hali mbaya zaidi inakaribia kutokea, ambayo operesheni za kibinadamu haziwezi kukabilian anayo," ameonya mratibu wa kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kwa Maeneo ya Palestina, Lynn Hastings.

Gaza "inakailiwa na hali mbaya ya kibinadamu", shirika la Afya Duiani (WHO) limeonya. Kulingana na WHO, idadi ya hospitali zinazofanya kazi huko Gaza ilipungua kutoka 36 hadi 18 chini ya kipindi cha siku 60.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.