Pata taarifa kuu

Ukanda wa Gaza wakumbwa na mashambulizi ya anga, misaada kupelekwa Kaskazini haiwezekani

Katika sasisho lililochapishwa kwenye mtandao wa X, shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza kwamba maeneo yaliyo karibu majengo yake kumejaa wakimbizi na watu wanaokabiliwa njaa na haina uwezo wa kutoa misaada kwa wale ambao hawakuweza kutoroka kuelekea kusini.Β 

Makaburi yaliyoharibiwa katika kitongoji cha Fallujah cha Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Makaburi yaliyoharibiwa katika kitongoji cha Fallujah cha Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza. REUTERS - STRINGER
Matangazo ya kibiashara

UNRWA linaongeza kuwa hakuna chakula cha kununua, hata kwa wale ambao wana uwezo wa wa kununua.

Wakati huo huo Bunge la Israel limeidhinisha bajeti ya vita ambayo inaongeza shekeli bilioni 25.9 (dola bilioni 7) kwenye bajeti ya taifa. Fedha hizo za ziada zitasaidia kulipia gharama za vita vya Gaza, kama vile fidia kwa askari wa akiba na makazi ya dharura kwa wakimbizi wa ndani, shirika la habari la REUTERS liinaripoti. Marekebisho hayo, yaliyoidhinishwa na kura za wabunge 59 waliounga mkono na 45 waliopinga, yaliongeza bajeti ya mwaka 2023 hadi shekeli bilioni 510 (dola bilioni 139), msemaji wa Braza la Wawakilishi la Israel (Knesset) amesema.

Israel ambayo Inadhamiria kufanya vita vyake dhidi ya Hamas "hadi mwisho", inaongeza mashambulizi ya anga Alhamisi hii, Desemba 14 katika Ukanda wa Gaza ambapo idadi ya watu raia wanasalia katika hali mbaya zaidi. Nayo Marekani imemtuma mshauri wake wa usalama wa taifa mjini Jerusalem.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.