Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Uganda: Rais wa Iran aunga mkono sheria ya 'kupinga ushoga' na kukosoa nchi za Magharibi

Rais wa Iran Ebrahim Raisi alianza safari ya siku tatu barani Afrika Jumatano Julai 12. Katika ziara ya kwanza ya kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu barani humo katika kipindi cha miaka 11, alizuru Kenya mara ya kwanza asubuhi na kisha katika nchi jirani ya Uganda mchana ambapo alikutana na mwenzake Yoweri Museveni. Fursa ya kuunga mkono masuala kadhaa, kuanzia sheria ya "kupinga ushoga ya mwaka 2023" iliyotangazwa Mei 29 na Kampala.

Rais wa Uganda Yoweri Museveni akimpokea na kumuonyesha njia mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi, mjini Kampala Julai 12, 2023.
Rais wa Uganda Yoweri Museveni akimpokea na kumuonyesha njia mwenzake wa Iran Ebrahim Raisi, mjini Kampala Julai 12, 2023. © Abubaker Lubowa / Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Nchi za Magharibi zinajaribu leo ​​kuendeleza wazo la ushoga, na kwa kulikuza, wanajaribu kukomesha aina ya binadamu," amesema rais wa Iran Ebrahim Raïsi: Rais wa Irani alizungumza kutoka Kampala, mwezi mmoja na nusu baada kutangazwa kwa sheria ya "kupinga ushoga" ambayo ilikuwa na uhusiano mbaya kati ya Uganda na washirika wake wa Magharibi.

Yaliyomo katika sheria hiyo yanachukuliwa kuwa moja ya kandamizi zaidi ulimwenguni: inatoa adhabu ambayo inaweza kwenda hadi adhabu ya kifo na inakataza "kuendeleza" kwa ushoga.

Mnamo Mei 29, saa chache baada ya sheria hii mpya, nchi kadhaa, pamoja na Maekai, ziliahidi mara moja vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Uganda.

Kutokana na mfululizo huu wa misimamo ya Magharibi, Kampala ilionysha msimamo wake: "Nchi za Magharibi hazitakuja kutawala nchi yetu", alitangaza spika wa bunge la Uganda. Siku ya Jumatano, rais wa Iran kwa alionyesha uungaji wake mkono kwa mwenyeji wake, Rais Museveni akithibitisha kwamba "nchi za Magharibi zinafanya kinyume na urithi wa tamaduni na mataifa".

Matamshi haya yanakuja katika muktadha wa ziara iliyoanzishwa na Ebrahim Raïssi barani Afrika. Ziara iliyotangazwa kama "mwanzo mpya na nchi" za bara. Hii sio tu kwa kiwango cha uchumi, lakini pia kwa mtazamo wa "maono ya kawaida ya kisiasa".

Rais wa Iran, ambaye alizungumza Jumatano asubuhi mjini Nairobi na mwenzake wa Kenya William Ruto, aliwasili alasiri huko Entebbe nchini Uganda. Anatarajiwa kusafiri hadi Harare nchini Zimbabwe siku ya Alhamisi kukutana na Rais Emmerson Mnangagwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.