Pata taarifa kuu

Rwanda: Mmoja wa watu wa mwisho wanaosakwa kwa mauaji ya halaiki akamatwa Afrika Kusini

Fulgence Kayishema, mmoja wa watuhumiwa wanne wa mwisho waliokuwa wanatafutwa kwa jukumu lao katika mauaji ya kimbari ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994, aanashikiliwa tangu siku ya Jumatano nchini Afrika Kusini, waendesha mashtaka wa Umoja wa Mataifa wanaochunguza kesi hiyo wamesema leo Alhamisi. 

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Bw. Kayishema, aliyezaliwa mwaka 1961, aliua ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 2,000 wakimbizi wanaume, wanawake, wazee na watoto katika kanisa la Nyange, katika wilaya ya Kivumu, Aprili 15, 1994.
Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Bw. Kayishema, aliyezaliwa mwaka 1961, aliua ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 2,000 wakimbizi wanaume, wanawake, wazee na watoto katika kanisa la Nyange, katika wilaya ya Kivumu, Aprili 15, 1994. © US State Department via Reuters
Matangazo ya kibiashara

"Mmoja wa watu wanaosakwa zaidi duniani (...) amekamatwa huko Paarl, Afrika Kusini", kama sehemu ya operesheni na mamlaka ya Afrika Kusini. Hayo yamesemwa na mahakama ya Umoja wa Mataifa katika taarifa yake.

Mtu huyo alitumia majina mengi bandia na hati za uwongo kuficha utambulisho wake na uwepo wake.

Alikuwa mmoja wa watuhumiwa wanne wa mwisho wanaotafutwa kwa jukumu lao katika mauaji ya halaiki dhidi ya Watutsi nchini Rwanda mwaka 1994. Fulgence Kayishema alikamatwa Jumatano (24 Mei) nchini Afrika Kusini, kulingana na waendesha mashtaka wa Umoja wa Mataifa wanaochunguza kesi hiyo.

 Fulgence Kayishema amekuwa mafichoni tangu mwaka 2001, imesema Taasisi ya Kimataifa Inayoshughulikia Masuala Yaliyosalia ya Mahakama kuhuiana na Makosa Ya Jinai (Mechanism), yenye jukumu la kukamilisha kazi ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu nchini Rwanda (ICTR).

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, Bw. Kayishema, aliyezaliwa mwaka 1961, aliua ikiwa ni pamoja na watu wengine zaidi ya 2,000 wakimbizi wanaume, wanawake, wazee na watoto katika kanisa la Nyange, katika wilaya ya Kivumu, Aprili 15, 1994.

Inadaiwa "alishiriki moja kwa moja katika kupanga na kutekeleza mauaji haya," mahakama imesema, "ikiwa ni pamoja na kununua na kusambaza petroli ili kuchoma kanisa na wakimbizi waliokimbilia ndani ya kanisa." “Hilo liliposhindikana, Bw. Kayishema na wengine walitumia tingatinga kuangusha kanisa, kuwazika na kuwaua wakimbizi waliokuwa ndani,” mahakama imeongeza.

Bw. Kayishema, anayeshtakiwa kwa mauaji ya halaiki, kushiriki katika mauaji ya halaiki, njama ya kufanya mauaji ya halaiki na uhalifu dhidi ya binadamu, alitumia majina mengi ya bandia na nyaraka za uongo kuficha utambulisho wake na uwepo wake, Mechanism imesema.

ICTR iliwatia hatiani jumla ya watu 62. Wengine, kama Augustin Bizimana, mmoja wa waandalizi wakuu wa mauaji hayo, walikufa bila kukabiliwa na mahakama ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.