Pata taarifa kuu

Mauaji ya Kimbari ya Watutsi nchini Rwanda: Rais Paul Kagame atoa onyo wakati wa maadhimisho

Miaka 29 baadaye, Rwanda inaadhimisha Aprili 7, 2023 mwanzo wa mauaji ya kimbari ya Watutsi. Miezi mitatu ya mauaji ambayo yalianza baada ya shambulio la ndege ya Rais Juvénal Habyarimana jioni ya Aprili 6, 1994 na kusababisha vifo vya takriban watu 800,000, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa. Kama kila mwaka, sherehe rasmi, iliyoandaliwa katika ukumbusho wa kitaifa wa Gisozi huko Kigali, imezindua siku 100 za kutafakari. Hafla ambayo Rais Paul Kagame amelihutubia taifa.

Rais wa Rwanda Paul Kagame akitoa hotuba wakati wa sherehe za za kuadhimisha miaka 29 ya ukumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya 1994 kwenye ukumbusho wa mauaji ya kimbari wa Gisozi mjini Kigali Aprili 7, 2023.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akitoa hotuba wakati wa sherehe za za kuadhimisha miaka 29 ya ukumbukumbu ya mauaji ya halaiki ya 1994 kwenye ukumbusho wa mauaji ya kimbari wa Gisozi mjini Kigali Aprili 7, 2023. AFP - MARIAM KONE
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Kigali, Lucie Mouillaud

Baada ya kuwasha mwenge wa kumbukumbu, Rais Paul Kagame alizungumza kwa kuwaenzi wahanga wa mauaji ya kimbari. “Tunaweza kusamehe, lakini hatuwezi kusahau,” amesema, pia akitoa onyo kwa umati wa watu waliokuwa wakimsikiliza.

"Hatuwezi, hata hivyo, kupuuza kwamba vurugu na matamshi ya chuki yanaendelea, sio mbali sana na hapa. Na licha ya hilo, tunaweza pia kuona leo mambo kama yale tuliyoona mwaka wa 1994.”

Kigali mara kwa mara inashutumu vitendo vya kundi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR), waasi wa Kihutu wanaoendesha harakati zao mashariki mwa DRC tangu kumalizika kwa mauaji ya kimbari ya 1994 dhidi ya Watutsi nchini Rwanda. Rais Paul Kagame amesema, 'ni muhimu kutosahau yaliyopita'.

“Kukana mauaji ya kimbari ni jaribio la hatari na la makusudi kuzuia ukweli. Ni lazima tupambane na itikadi kama hii, kwa sababu itikadi hii inasambazwa kwa urahisi kutoka kizazi hadi kizazi, na lazima tupambane na kukataa mauaji ya kimbari kwa sababu ndivyo historia inavyojirudia. »

Maadhimisho yataendelea kote nchini kwa siku 100 kuwaezi wahanga wa mauaji ya kimbari, hadi Juni 3. Siku mia moja ambapo mwali wa ukumbusho, katika kumbukumbu ya waliotoweka, utaendelea kuwaka katika ukumbusho wa Gisozi, ambapo zaidi ya wahanga 250,000 wamezikwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.