Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Mashariki mwa DR Congo: Mapigano kati ya jeshi na M23 yarindima karibu na Sake

Mapigano kati ya jeshi na waasi wa M23 yanaripotiwa kwenye barabara inayounganisha Sake na Butembo, karibu na Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini. Hali ya mambo mashariki mwa DRC itakuwa kiini cha mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaotarajiwa kufanyika Jumamosi, Februari 4, mjini Bujumbura. Wanaotarajiwa hasa ni Rais wa Kongo Félix Tshisekedi na Rais wa Rwanda Paul Kagame, ambao hawajakutana tangu mwezi Septemba.

Mji wa Sake, ambako mapigano yanaelekea.
Mji wa Sake, ambako mapigano yanaelekea. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kunaripotiwa mapigano kati ya wanajeshi wa DRC (FARDC) na M23 kwenye barabara inayounganisha Sake na Butembo. Kwa usahihi zaidi, mapigano kwa leo Ijumaa yanaripotiwa kilomita thelathini kaskazini mwa mji wa Sake.

Kwa wachambuzi wengi, Sake ni eneo linalofuata kulengwa na kundi hili la waasi ambao wengi wao ni kutoka kabila la Watutsi. Kwa hakika, kutekwa kwa jiji hili muhimu kutaitenga kabisa Goma, mji mkuu wa mkoa wa Kivu Kaskazini. Hali inayoogopwa hasa na mashirika ya kiraia, ambayo yanabaini kuwa kutakuwa na ugumu wa usambazaji wa chakula kwa wakaazi wa mji huo na kuonya juu ya mzozo wa kibinadamu unaoendelea katika mkoa huo.

Kila kunakoripotiwa mapigano, raia wengi huyatoroka makaazi yao na wengi kukimbilia maeneo salama. Vijiji kwenye lango la Masisi viko tupo, anaelezea ofisa wa mashirika ya kiraia na kwa sasa hakuna msaada kwa watu hawa wanaozidi kuhama makazi yao, ameongeza.

Tarehe 3 Februari MONUSCO, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC, umetangaza kwamba utatoa ulinzi kwxa msafara ambao unatarajia kuondoka kutoka Goma hadi Kitshanga, mji ambao waasi waliuteka wiki iliyopita. Lengo: kuleta chakula na vifaa vya matibabu kwa watu waliokimbia makazi yao ambao wamepata hifadhi ndani na karibu na kambi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa.

Felix Tshisekedi na Paul Kagame wanatarajiwa katika mkutano wa kilele mjini Bujumbura

Hali ya Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo itakuwa kiini cha mkutano wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) unaotarajiwa kufanyika Jumamosi hii Februari 4, 2023 mjini Bujumbura, nchini Burundi. Marais wote wa eneo hilo wanatarajiwa, akiwemo rais wa DRC Félix Tshisekedi na wa mwenzake wa Rwanda Paul Kagame, ambao hawajakutana tangu mwezi Septemba 2022, baada ya kukukatan mjini New York.

Nchi hizo mbili zimekuwa katika mzozo tangu kurejea kwa waasi wa M23 wenye silaha huko Kivu Kaskazini zaidi ya mwaka mmoja uliopita. Mchakato uliotiwa saini mjini Luanda mwezi Novemba ulikuwa wa kufikia usitishaji mapigano na kuwaondoa waasi katika maeneo yanayokaliwa. Hali ambayo sivyo ilivyo leo.

Usitishaji mapigano kati ya M23 na FARDC, ambao ulikuwa bado unaendelea kidogo, ulivunjwa kabisa mwezi wa Januari wakati waasi walipofikia baada ya Rutshuru, eneo la Masisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.