Pata taarifa kuu
DRC: ZIARA YA PAPA FRANCIS

Papa atoa wito kwa wahusika wa mauaji ni DRC kuchukuliwa hatua

Wakati huu kiongozi wa kanisa katoliki, duniani Papa Francis, akiwa amehitimisha ziara yake nchini DRC, amewataka viongozi wa nchi hiyo kuhakikisha wahusika wa vitendo vya ubakaji na mauaji, wanafikishwa katika vyombo vya sheria.

Ziara ya Papa Francis nchini DR Congo
Ziara ya Papa Francis nchini DR Congo AP - Jerome Delay
Matangazo ya kibiashara

Sébastien Muyengo, ni askofu wa Uvira, na hapa anaeleza kile ambacho Papa alikisisitiza kwa raia wa Mashariki, kama alivyohojiwa na mwenzetu Véronique Gaymard.

“Tulipenda Papa mwenyewe ahisi na onyeshwe hali ilivyo kwa sababu taarifa zinapowafikia kule ulaya hawaamini kuwa mtu anaweza kukatwa shingo kama mnyama. ” ameeleza Sébastien Muyengo

Papa Francis amekuwa nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo kwa ziara ya siku tatu akihubiri injili ya upendo, amani na msamaha, akiwataka raia waliokosewa kutoa msamaha kama njia moja ya kuiga mfano wa Yesu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.