Pata taarifa kuu
DRC: ZIARA YA PAPA FRANCIS

DRC: Papa Francis, amekutana na waathiriwa wa machafuko

Papa Francis, Jumatano alikutana na kuzungumza na waathiriwa wa machafuko yanayoendelea Mashariki mwa DRC, na kulaani mateso yanayoendelea kuwapata raia wasiokuwa na hatia mikononi mwa makundi ya waasi.

Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis anaendelea na ziara yake nchini DRC kabla ya kuelekea Sudan Kusini.
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis anaendelea na ziara yake nchini DRC kabla ya kuelekea Sudan Kusini. via REUTERS - VATICAN MEDIA
Matangazo ya kibiashara

Mama huyu ni mmoja wa waathiriwa 50, waliokutana na Papa, yeye anatokea Uvira, huko Kivu Kusini, alimwambia mwenzetu wa RFI Kifaransa Veronique Gaymard, walichomwambia Papa Francis. 

“Hapa tumefurahia kwa sababu tunatafuta amani, kwa sababu kwetu tunaishi kwa vita vikubwa sana, tuliporwa, tulifanyiwa mambo mengi tu na tukakimbia.” amesema mmoja wa waathiriwa. 

Nchi ya DRC ambayo asilimia kubwa ya raia wake ni waumini wa kanisa Katoliki wanamatumaini kuwa ziara ya kiongozi huyo wa dini itasaidia katika upatikanaji wa amani eneo la Mashariki.

"Kwa uchungu moyoni mwangu, naomba Mungu asamehe ukatili wa mwanadamu dhidi ya mwanadamu. Baba, utuhurumie, Wafariji wahasiriwa na wanaoteseka. Uongoze mioyo ya wale wanaofanya ukatili wa kikatili unaoleta aibu kwa wanadamu wote."amesema Papa Francis.

Papa Francis anaendelea na ziara yake Alhamis, kabla ya kuelekea nchini Sudan Kusini siku ya Ijuma. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.