Pata taarifa kuu
USALAMA-MIUNDOMBINU

Watu kumi wafariki katika ajali ya barabarani mashariki mwa DRC

Watu kumi wamefariki dunia mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo siku ya Ijumaa wakati gari lililowabeba lilipopinduka kutokana na mizigo kupita kiasi na hali mbaya ya barabara, mamlaka ya mkoa imesema.

Gari hili ambalo pia lilikuwa likisafirisha mizigo, liliondoka katika soko la Kiziba katika eneo la Shabunda kuelekea Mwenga, katika eneo lisilo na bandari la mkoa wa Kivu Kusini.
Gari hili ambalo pia lilikuwa likisafirisha mizigo, liliondoka katika soko la Kiziba katika eneo la Shabunda kuelekea Mwenga, katika eneo lisilo na bandari la mkoa wa Kivu Kusini. L. Mouaoued/RFI
Matangazo ya kibiashara

Gari hili ambalo pia lilikuwa likisafirisha mizigo, liliondoka katika soko la Kiziba katika eneo la Shabunda kuelekea Mwenga, katika eneo lisilo na bandari la mkoa wa Kivu Kusini.

Ajali hiyo imesababisha "vifo vya watu kumi na wengine kadhaa kujeruhiwa, waathriwa wote ni abiria (wanaume na wanawake) waliokuwa kwenye lori," Waziri wa Mambo ya Ndani na Usalama katika mkoa wa Kivu Kusini Théophile Kiluwe Migo ameliambia shirika la habari la AFP.

"Kupakia kupita kiasi na ubovu wa barabara ndio chanzo cha ajali hii, gari imepinduka" kwenye barabara ya taifa namba 2, amebaini.

Ni "lori aina ya Mercedes Benz lililokuwa limebeba abiria na bidhaa kadhaa (ambalo) lilipinduka mapema" Ijumaa asubuhi katika kijiji cha Kitongo huko Kivu Kusini, Hilaire Isombya, kiogozi wa shirika la kiraia huko Mwenga ameliambia shirika kla habari la AFP. Amebaini kwamba wahanga ni 'wanaume 6 na wanawake wanne'.

Nchini DRC, nchi kubwa yenye kilomita za mraba milioni 2.3 ambayo ina barabara chache zinazopitika, ajali nyingi zinaripotiwa, na mara nyingi hasara ni kubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.