Pata taarifa kuu

Mlipuko wa lori la mafuta nchini DRC waua watu kadhaa

Mlipuko wa lori lililokuwa limesheheni mafuta umesababisha "vifo kadhaa na wengine kuungua vibaya" usiku wa Jumatano kuamkia Alhamisi magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Gavana wa jimbo la Kongo Central ametangaza.

Mnamo 2010, mlipuko wa lori uliua zaidi ya watu 230 na kujeruhi karibu watu 100 nchini DRC.
Mnamo 2010, mlipuko wa lori uliua zaidi ya watu 230 na kujeruhi karibu watu 100 nchini DRC. RFI / SΓ©bastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ripoti mbalimbali zinasema watu 9 mpaka 50 wamepoteza maisha kwa kuteketea, na wengine zaidi ya 20 wamejeruhiwa,Β Β baada ya lori liliokuwa limebeba mafuta kulipuka katika jimbo laΒ Β Kongo CentralΒ katika kijiji cha Mbuba, umbali wa Kilomita 120 kutoka jiji kuu Kinshasa.

Ajali hiyo, ambayo bado haijafahamika, ilitokea katika barabara kuu ya taifa namba 1, karibu na kijiji cha Mbuba, katika eneo la Madimba, kilomita 120 magharibi mwa mji wa Kinshasa. Kulingana na vyanzo kutoka mashirika ya kiraia, gari hilo lilikuwa likielekea mji mkuu wa Kongo na lililipuka karibu na soko dogo.

"Kumeripotiwa vifo kadhaa na watu wengine kuungua vibaya huko Mbuba jioni ya leo baada ya mlipuko wa lori kwenye barabara kuu RN-1", alibainisha kwenye Twitter gavana wa mkoa wa Kongo Central, Guy Bandu.

Hakuna ripoti nyingine iliyotolewa mapema Alhamisi asubuhi.

"Ni wakati mwafaka wa kuchukua hatua kali na za kijasiri kuimarisha udhibiti wa usafiri, hasa wa bidhaa zinazoweza kusababisha hatari ya kuzuka kwa moto, ili kukomesha matukio kama hayo yanayotokea mara kwa mara. Barabara kuu ya kitaifa RN1 haipaswi kuwa makaburi", aliongeza Gavana kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Barabara RN1 inaunganisha Kinshasa na vituo pekee vya baharini vya DRC, Matadi na Boma.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.