Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Kinshasa: Watu 25 wauawa na umeme nje ya soko la Matadi Kibala

Takriban watu ishirini na watano, wengi wao wakiwa wachuuzi katika soko la Matadi Kibala (magharibi mwa mkoa wa Kinshasa), wamefariki dunia baada ya kupigwa na umeme kutokana na kukatika kwa waya ya umeme unaosafirisha kiwango kikubwa cha umeme Jumatano, Februari 2.

Kamanda wa polisi katika wilaya ya Lukunga, Kanali Lili Tambwe, amesema kuwa wahanga hao walikuwa katika soko lisilo julikana rasmi lililowekwa kando ya barabara kwenye lango la soko la Matadi Kibala.
Kamanda wa polisi katika wilaya ya Lukunga, Kanali Lili Tambwe, amesema kuwa wahanga hao walikuwa katika soko lisilo julikana rasmi lililowekwa kando ya barabara kwenye lango la soko la Matadi Kibala. Arsene Mpiana AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Idadi hii bado ni ya muda na imetangazwa na polisi. Kulingana na ujumbe wa Twitter kutoka kwa afisa wa mawasiliano wa gavana wa jiji la Kinshasa, miili ishirini na sita imepelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.

Mkuu wa polisi katika wilaya ya Lukunga, Kanali Lili Tambwe, akinukuliwa na Radio OKAPI, amesema kuwa wahanga hao walikuwa katika soko lisilo julikana rasmi lililowekwa kando ya barabara kwenye lango la soko la Matadi Kibala.

Ni waya ya umeme unaosafirisha kiwango kikubwa cha umeme ndio uliyosababisha tukio hili la kusikitisha baada ya kukatika na kuanguka kwenye soko lisilo julikana rasmi. Si sokoni Matadi Kibala. Wahanga ni wachuuzi. Jumla ya waliofariki ni 25, wakiwemo wanawake 23 na wanaume wawili. Wanawake wawili walionusurika walipelekwa kwenye kituo cha afya.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa saa chache baada ya kutokea kwa mkasa huo, Shirika la Umeme nchini DRC (SNEL) limeeleza kuwa, wakati wa mvua iliyonyesha katika jiji la Kinshasa, radi ilipiga moja ya waya za umeme na kusababisha kukatika, na hivyo kuanguka katika soko la Matadi Kibala”.

Aidha, Waziri Mkuu, Gavana wa jiji la Kinshasa, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Masuala ya Kibinadamu na Mkuu wa polisi katika mkoa wa Kinshasa wamezuru eneo la tukio.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.