Pata taarifa kuu
DRC-UCHUNGUZI

DRC: Tume ya uchunguzi kufahamu sababu za ajali ya treni

Ripoti rasmi ya ajali ya treni huko Katanga inaripoti kuwa watu 75 wamefariki dunia, 125 kujeruhiwa ikiwa ni pamoja na 28 waliopatwa na kiwewe.

Dereva wa treni huko Kananga kusini mwa DRC mwaka wa 2007.
Dereva wa treni huko Kananga kusini mwa DRC mwaka wa 2007. AFP - LIONEL HEALING
Matangazo ya kibiashara

Mamlaka imeweka tume ya uchunguzi, huku baadhi ya mabehewa bado hayajatambuliwa. Inawezekana kwamba miili mingine ya abiria bado iko chini ya tani za vyuma chakavu. Shirika la reli inadai kuwa abiria hawa walikuwa hawajulikani rasmi.

Wachunguzi hao wakiongozwa na Marc Manyanga Ndambo, mkurugenzi wa miundombinu wa shirika la Kitaifa la Reli nchini DRC (SNCC) wameanza kusikilizwa.

Kwanza kwa abiria kuelewa jinsi walivyopanda treni ya mizigo. Lakini kwa upande wa mkuu wa tume ya uchunguzi, utambuzi wa kiufundi pia ni muhimu: "Kuna maswali na kuna uchunguzi wa kiufundi kabisa ili kujaribu kuelewa kwa nini ajali hii, kwa nini kulikuwa na sintofahammu. Kutafanyika uchunguzi wa kina kuhusu treni hiyo ili kujaribu kuelewa kilichotokea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.