Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Watu watano wapoteza maisha katika ajali ya ndege ndogo Shabunda

Watu watano walifariki dunia baada ya ndege waliokuwemo kuanguka Alhamisi hii, Desemba 23, 2021 katika eneo la Shabunda, katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Ukungu kutokana na hali mbaya ya hewa ndio chanzo cha ajali ya chombo hiki.

Shabunda, Kivu Kusini: Ujumbe wa ukaguzi uliofanywa mwaka 2016 na MONUSCO katika maeneo duni ya DRC.
Shabunda, Kivu Kusini: Ujumbe wa ukaguzi uliofanywa mwaka 2016 na MONUSCO katika maeneo duni ya DRC. MONUSCO / Taimoor
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mkuu wa eneo la Shabunda, ndege ndogo kutoka kampuni ya Malu Aviation ndio ilianguka msituni dakika sita kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Shabunda.

Ndege hiyo iliyokuwa ikitokea mjini Goma, ilikuwa ikisafirisha bidhaa: kwa sehemu kubwa, vyakula katika msimu huu wa sikukuu.

Kashombana Bin Saleh anabainisha kuwa rubani kutoka Ubelgiji, rubani msaidizi, wafanyakazi mmoja na abiria wawili ni miongoni mwa wahanga.

Anaongeza kuwa ndege hiyo ilipatikana karibu na kijiji cha Mupasa, na sio katika kijiji cha Keisha kama ilivyotangazwa hapo awali.

Akitoa rambirambi kwa familia za wahanga, Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano katika mkoa wa Kivu Kusini, Alimasi Malumbi Matthieu, amebanini kwamba shughuli ya kutafuta kisanduku cheusi, ili kubaini sababu za ajali hiyo, inaendelea.

Siku nne zilizopita, mwanamke mwenye ulemavu wa kusikia alifariki dunia baada ya kugongwa na ndege ndogo kwenye uwanja wa ndege wa Shabunda.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.