Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC: Watu kadhaa wafariki dunia baada ya meli mbili kugingana katika Mto Congo

Watu kadhaa wamefariki dunia katika ajali iliyotokea kwenye Mto Congo, baada ya meli mbili kugongana uso kwa uso siku ya Jumatano, Novemba 17 usiku. Vyanzo vya usalama kutoka N'sele na serikali ya mkoa vinabaini kwamba watu kadhaa hawajulikani waliko, bila kutoka maelezo zaidi.

Safari za meli wakati wa usiku zimepigwa marufuku na mamlaka katika sehemu tofauti za nchi, lakini hatua hiyo mara nyingi inakabiliwa na ukosefu wa utekelezaji.
Safari za meli wakati wa usiku zimepigwa marufuku na mamlaka katika sehemu tofauti za nchi, lakini hatua hiyo mara nyingi inakabiliwa na ukosefu wa utekelezaji. Youtube
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na vyanzo hivi, Meli iitwayo Sanza na Moi na nyingine iitwayo Emmanuel, ziligongana mwendo wa saa tatu usiku, katika eneo la Mambutuka, kwenye Mto Congo, si mbali na makutano kati ya Mto Kasai na Mto Congo.

Watu wachache walionusurika wamefika mjini Kinshasa, kulingana na mjumbe wa serikali ya mkoa ambaye alihojiwa na Radio Okapi nchini humo.

Zoezi la utafutaji wa abiria waliokosekana linaendelea na kukusanya habari ili kujua kilichotokea.

Safari za meli wakati wa usiku zimepigwa marufuku na mamlaka katika sehemu tofauti za nchi, lakini hatua hiyo mara nyingi inakabiliwa na ukosefu wa utekelezaji.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.