Pata taarifa kuu
DRC

Watu 25 wapoteza maisha nchini DRC baada ya kuzama kwa boti

Watu 25 wanahofiwa kupoteza maisha nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya boti waliyokuwa wanasafiri kuzama katika mto Congo, mkoani Tshopo, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Ziwa Albert kati ya Uganda na DRC
Ziwa Albert kati ya Uganda na DRC FILE PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Naibu Gavana wa mkoa wa Thsopo Maurice Abibu Sakapela, amesema tayari milli ya watu sita imepâtiikana, watu wengine 237 wameokolewa lakini wengine 19 hawajapatikana.

Uongozi wa mkoa huo umesema boti hiyo ilizama Ijumaa iliyopita, baada ya kutokea Kisangani kwenda Basoko.

Aidha, Sakapela ameliambia Shirika la Habari la Ufaransa AFP kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni abiria na mizigo kupita kiasi na wanaoaminiwa kuhusika wamekamatwa wakati huu uchunguzi ukiendelea.

Ajali za boti, ni kawaida nchini DRC kutokana na watu nchini humo kutumia usafiri wa majini kwa sababu ya ukosefu wa barabara na reli.

Mikasa kama hii pia imewahi kuripotiwa katika Ziwa Albert.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.