Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

DRC : Idadi ya watu waliofariki katika ajali ya treni Buyofwe yaongezeka

Idadi ya waliofariki katika ajali ya treni ya mizigo kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hapo jana imeongezeka kutoka watu sita hadi watu kumi baada ya miili mingine kugunduliwa katika eneo la tukio.

Idadi rasmi ya watu waliokuwa ndani ya treni hii haijajulikana. Kutokana na ukosefu wa njia ya gari, Raia wa eneo hilo husafiri na treni, huku miondombinu ya reli ikiwa ni ile ya wakati wa ukoloni na haifanyiwi ukarabati.
Idadi rasmi ya watu waliokuwa ndani ya treni hii haijajulikana. Kutokana na ukosefu wa njia ya gari, Raia wa eneo hilo husafiri na treni, huku miondombinu ya reli ikiwa ni ile ya wakati wa ukoloni na haifanyiwi ukarabati. AFP/Archivos
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na shirika la msalaba mwekundu eneo la Lualaba ambapo ajali hio ilifanyika, maiti tayari zmezikwa na  raia zaidi ya ishirini na mbili wamelazwa katika hosptali.

Baada ya timu mafundi na madaktari kufika eneo la tukio huko Buyofwe, wamesema kuwa treni ambayo ilikuwa na mabehewa 8 ilipoteza njia na kusababisha watu hawa kupoteza maisha.

"wakati tulipofika hapa kulikuwa miili mingi na tumezika miili yote na kila moja na kaburi lake sababu atukutaka kufanya kaburi la pamoja " , amesema mmoja wa maafisa wa shirika la Mslaba mwekundu. 

Mashirika ya kiraia yanaendelea kulaumu shirika la SNCC, shirika la reli la serikali kuhusika na ajali hizi ambazo zimeripotiwa kila mara chini DRC.

"Tunasikitika kila mara na ajali hizi za treni kutokana na uzembe wa SNCC ambayo reli zake ni zatangu ukoloni na mbovu, tunaomba serikali kusimamisha treni zote hizo za zamani na kuwaachisha kazi wafanyakazi wote ambao wamezeheka" , amesema Fulbert Ngoyi Kitwamwele, kiongozi wa shirika la kiraia.

Hata hivyo idadi rasmi ya watu waliokuwa ndani ya treni hii haijajulikana. Kutokana na ukosefu wa njia ya gari, Raia wa eneo hilo husafiri na treni, huku miondombinu ya reli ikiwa ni ile ya wakati wa ukoloni na haifanyiwi ukarabati.

Taarifa ya Freddy Tendilonge

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.