Pata taarifa kuu

DRC: Watu 34 wafariki wakiwemo watoto 16 katika ajali ya barabarani huko Lualaba

Gari hilo lilikuwa limeondoka Mbuji-Mayi, katika jimbo la Kasai-Oriental na lilikuwa likielekea Kolwezi, mji mkuu wa Lualaba.

Mwaka 2010, mlipuko wa lori la mafuta uligharimu maisha ya zaidi ya watu 230 na mamia waliojeruhiwa nchini  RDC.
Mwaka 2010, mlipuko wa lori la mafuta uligharimu maisha ya zaidi ya watu 230 na mamia waliojeruhiwa nchini RDC. RFI / Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Watu 34 wakiwemo watoto 16 walifariki dunia Jumatatu katika ajali ya lori la mizigo, ambalo pia lilikuwa likisafirisha abiria, kwenye barabara katika eneo lisilo na bandari kusini-mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kulingana na mamlaka katika eneo hilo.

Lori hilo lililokuwa limepakia basi dogo, mizigo na abiria 93, lilishindwa kupanda mlima na kupinduka,  amesema Lundanda Panga, msimamizi wa eneo la Lubudi, akilielezea shirika la habari la AFP,  katika jimbo la Lualaba, akihojiwa kwa njia ya simu kutoka Lubumbashi, jiji jirani la Haut-Katanga.

“Watu 33 walikufa papo hapo, tuliwazika jana (Jumanne) kwenye kaburi la pamoja, kwani miili yao ilikuwa tayari inaoza” kutokana na joto hilo, alisema. "Mwanamke wa umri wa miaka thelathini aliyefariki hospitalini Jumanne kutokana na majeraha yake amezikwa leo (Jumatano)," Bi Lundanda ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.