Pata taarifa kuu

Wanandoa wa Marekani washtakiwa Uganda kwa 'biashara haramu ya watoto'

Wanandoa wa Kimarekani wamefunguliwa mashtaka nchini Uganda kwa "biashara haramu ya watoto", wiki moja baada ya kufunguliwa mashitaka kwa "mateso makali" ya mtoto wao wa kulea mwenye umri wa miaka 10, kulingana na uamuzi wa mahakama ya Uganda siku ya Jumanne, ambao ulikataa ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana.

Moja ya maeneo ya mji wa Kampala, Uganda.
Moja ya maeneo ya mji wa Kampala, Uganda. AFP - BADRU KATUMBA
Matangazo ya kibiashara

Mwanamume na mwanamke, wote 32, walishtakiwa mnamo Desemba 9 kwa "mateso ya hali ya juu" na kupelekwa katika Gereza la Luzira, gereza lenye ulinzi mkali nje kidogo ya mji mkuu Kampala.

Wanandoa hao walishtakiwa Jumanne kwa "biashara haramu wa watoto uliokithiri", kulingana na uamuzi wa mwendesha mashtaka Joan Keke. Hakimu wa Uganda pia alikataa ombi la kuachiliwa kwa dhamana.

"Hawana hatia", amejibu Leila Ghalibu, wakili wa wanandoa hao, kwa shirika la habari la AFP, akithibitisha kwamba mamlaka "hawana uthibitisho". Kesi inayofuata imeratibiwa Januari 18, 2023.

Kulingana na hati ya mashtaka, wanandoa hao "walimtesa kila mara" mtoto, akihudhuria kituo cha watu wenye ulemavu, kati ya 2020 na 2022. Mamlaka ziliarifiwa na majirani.

Wakati wa uvamizi kwenye nyumba ya wanandoa hao, polisi walipata video zinazoonyesha mtoto huyo alilazimishwa kuchuchumaa katika hali mbaya, akipewa chakula cha baridi tu na kulazwa kwenye "jukwaa la mbao, bila godoro au matandiko".

Mvulana huyo ni mmoja wa watoto watatu, aliyewasili wa wanandoa hao, ambaye alifika Uganda mwaka wa 2017 ili kujitolea katika shirika lisilo la faida lenye makao yake makuu nchini Marekani katika mji wa Jinja kabla ya kuhamia Naguru, kitongoji kikuu cha Kampala, kufanya kazi katika kuanzisha biashara.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.