Pata taarifa kuu
HAKI-USALAMA

Uganda: ICC yakataa rufaa ya mbabe wa zamani wa kivita wa LRA, Dominic Ongwen

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC, imetupilia mbali rufaa iliowasilishwa na kamanda wa zamani wa kundi la waasi la Uganda, Lord's Resistance Army LRA Dominic Ongwen kupinga hukumu aliopewa mwaka uliopita.

Majaji katika kitengo cha rufaa cha ICC wamekata rufaa ya kamanda wa zamani wa LRA Dominic Ongwen, aliyepatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Majaji katika kitengo cha rufaa cha ICC wamekata rufaa ya kamanda wa zamani wa LRA Dominic Ongwen, aliyepatikana na hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu. © ICC-CPI
Matangazo ya kibiashara

Ongwen aliwasilisha rufaa hiyo kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 25 jela kwa kutuhumiwa kutekeleza uhalifu wa kivita, baada ya mawakili wa utetezi mapema mwaka huu kudai kuwa hukumu ya Ongwen inapaswa kubatilishwa kwani aliathirika na masaibu mengi akiwa kama mwanajeshi mtoto.

Majaji wa mahaka ya rufaa katika uamizi wao walitupilia mbali hoja za Ongwen kuhusu maisha yake ya zamani kam mpiganaji noto na kwamba alikuwa na ugonjwa wa akili, na kusema kuwa Ongwen alikuwa na jukumu muhimu katika ukatili wa LRA akiwa mtu mzima.

Majaji hao aidha walisema kuwa Ongwen hakuathrika na matatizo ya akili licha  ya historia yake ya kutekwa akiwa mdogo.

Waendesha mashtaka walimuelezea Ongwen kama mtu aliyeongoza ugaidi wa kundi la LRA, kwa kuagiza mauaji ya zaidi ya watu 130 katika kambi za wakimbizi za Lukodi, Pajule, Odek na Abok kati ya mwaka wa 2002 na 2005.

Ongwen ambaye alitekwa nyara akiwa angali mtoto wa miaka tisa na kundi hilo la waasi lilikuwa chini ya uongozi wa Joseph Kony, mwaka uliopita, alipatikana na hatia ya mauaji, ubakaji na utumwa wa kingono kasakazini mwa Uganda mwanzoni mwa miaka ya 2000.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.