Pata taarifa kuu
ICC-HAKI

Uganda: Dominic Ongwen azungumza kwa mara ya kwanza katika kesi yake ICC

Dominic Ongwen amevunja ukimya wake na kuuthibitishia ulimwengu kwamba uhalifu anaotuhumiwa aliufanya chini ya maagizo ya kiongozi wake Joesph Kony.

Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha waasi wa Uganda, LRA, Dominic Ongwen, akiwa katika mahakama ya ICC, 6 December 2016.
Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha waasi wa Uganda, LRA, Dominic Ongwen, akiwa katika mahakama ya ICC, 6 December 2016. REUTERS/Peter Dejong/Pool
Matangazo ya kibiashara

Dominic Ongwen ambaye alikuwa mmoja wa viongozi wakuu wa kundi la waasi wa Uganda, LRA, anakabiliwa namashitaka huko Hague mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, ambayo ilimpata na hatia mwanzoni mwa mwezi wa Februari ya makosa 61 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanywa kaskazini mwa Uganda kati ya mwaka 2002 na 2005.

Kesi yake imeendelea kusikilizwa tangu Jumatano wiki hii. Hata hivyo mshirika huyo wa karibu wa Joseph Kony amesimulia kilichomkuta kabla ya kujiunga na kundi la waasi la LRA, lakini anajutia aliyoyafanya akiwa katika kundi hilo.

Dominic Ongwen amezungumza kwa karibu saa mbili. Hali ambayoimewashangaza wengi baada ya miezi kadhaa kukataa kutoa ukweli wake kuhusu shutma dhidi yake. "Sikujisikia vizuri wakati wa kesi," amesema.

Dominic Ongwen ajutia makosa yake

Ameelezea jinsi alivyotekwa nyara na wapiganaji wa Joseph Kony mnamo mwaka 1987 alipokuwa akienda shule. Pia amesimulia Jinsi, baada ya jaribio la kutoroka, alipewa panga, na kuua wafungwa, akilazimishwa kunywa damu yao na kula  matumbo yaliyochanganywa na maharagwe.

Kwa miaka mingi kijana huyo alibadili tabia akiwa katika kundi la LRA na kuwa muuaji hatari, kwa kipindi cha miaka 27,chini ya maagizo ya Joseph Kony "aliye na pepo wachafu, amesema." "Nilipigwa risasi kumi na moja," amesema, "sina bahati ya kuwa sijafa. "

Dominic Ongwen ajaribu kujitetea

"Nilijisalimisha, niliomba ulimwengu unisaidie." Anasema alijihusisha sana na mambo ya dini na tiba ili kujaribu kushinda hofu ambayo bado inamzuia kulala. Majuto yake pia: "Siwezi kuomba msamaha kwa kila mtu au familia nilioikosea", "Mnisaidie, nirekebisheni, nifundishneni. Ninaweza kupambana, ndicho kitu pekee ninachojua. "

Mahakama kuchukuwa uamuzi

Mahakama italazimika kuamua ikiwa utetezi wake na safari yake ndefu kama mpiganaji wa zamani mtoto vitasaidia kwa kumlegezea hukumu ambayo angelipewa. Anakabiliwa na kifungo cha miaka thelathini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.