Pata taarifa kuu
UGANDA

ICC yamkuta Dominic Ongwen na hatia ya makosa ya kivita

Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za makosa ya uhalifu wa kivita ICC, imemkuta na hatia ya makossa ya uhalifu wa kivita na dhulma dhidi ya binadamu, mpiganaji wa zamani wa kundi la waasi wa Lords Resistance Army, LRA la nchini Uganda, Dominic Ongwen.

Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha waasi wa Uganda, LRA, Dominic Ongwen, akiwa katika mahakama ya ICC, 6 December 2016
Aliyekuwa kamanda wa kikosi cha waasi wa Uganda, LRA, Dominic Ongwen, akiwa katika mahakama ya ICC, 6 December 2016 ICC media outlet
Matangazo ya kibiashara

Dominic Ongwen, mwenye umri wa miaka 45 hivi sasa amekutwa na hatia ya makosa 61 aliyoyatekeleza kuanzia mwaka 2000, likiwemo kosa la kulazimisha wanawake kupata ujauzito.

Mahakama hiyo imesema, Ongwen, aliagiza mashambulizi dhidi ya kambi za wakimbizi chini ya maelekezo ya kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony.

Miongoni mwa makosa mengine ambayo Ongwen aliyefahamika kwa jina jingine kama White Ant, amekutwa na hatia, ni pamoja na mauaji, ubakaji, utumwa wa ngono na kusajili watoto wadogo kwenye kundi lao.

Majaji wa mahakama hiyo walikataa hoja za mawakili wa utetezi waliodai kuwa mteja wao alikuwa muhanga baada ya kutekwa na wapiganaji wa LRA akiwa na umri wa miaka 9 na kwamba ameathirika kisaikolojia.

Tayari mashirika kadhaa ya kutetea haki za binadamu yamepongeza hukumu hiyo waliyosema ni ushindi kwa wahanga wa vitendo vya Ongweni.

Kundi la LRA liliundwa miongo mitatu iliyopita, na kijana aliyekuwa mtumishi wa kanisa katoliki na kujiita nabii, Joseph Kony, ambaye kwa miaka anadaiwa kuua watu zaidi ya laki moja na kuwateka watoto zaidi ya emfu 60 kwenye nchi za Sudan, DRC na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.