Pata taarifa kuu
ICC-UGANDA

ICC yamhukumu mbabe wa kivita Dominic Ongwen kifungo cha miaka 25

Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai ICC imemhukumu kifungo cha miaka 25 kiongozi wa zamani wa waasi wa Lord's Resistance Army,LRA Dominic Ongwen.

Dominic Ongwen, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Dominic Ongwen, mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC). REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Hukumu hiyo imetolewa muda mfupi uliopita na Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya uhalifu wa kivita ya mjini The Hague, Uholanzi.

Mbabe huyo wa kivita aliyeingizwa kwenye kundi la uasi akiwa mtoto alipanda ngazi na kufikia wadhifa wa kamanda wa kundi la waasi la Lord's Resistance Army, LRA la nchini Uganda.

Ongwen alikutwa na hatia ya mashitaka 61 mwezi Februari, yakiwemo ya mauaji, ubakaji na kuwatumikisha watu katika hali ya utumwa. 

Waendesha mashtaka wanasema kuwa Bw. Ongwen amepewa adhabu ndogo kwasababu alikuwa ametekwa na LRA akiwa mtoto mdogo.

Ongwen angelihukumiwa kifungo cha miaka 30 kulingana na ukubwa wa makosa

Waendesha mashitaka walitaka apewe kifungo cha miaka 20, kwa hoja kwamba kutekwa kwake akiwa mwanafunzi na kuingizwa katika kundi hilo la waasi, kunahalalisha kupunguziwa adhabu ambayo ingekuwa kifungo cha miaka 30 gerezani.

Alitekwa nyara na kundi la waasi wa Josephy Kony akiwa mvulana mdogo wakati akielekea shule ya msingi Abili Koro, kulingana na maelezo yake alidai alitekwa nyara mwaka 1988 akiwa na umri wa miaka 14.

Lakini ripoti sahihi zinasemekana alitekwanyara akiwa na umri wa miaka 9 au 10

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.