Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Wapiganaji 11 wa ADF wauawa baada ya kuingia Uganda

Wapiganaji 11 wa kundi la Allied Democratic Forces (ADF) wameuawa nchini Uganda baada ya kuvuka mpaka kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), jeshi la Uganda limesema siku ya Jumanne.

Wanajeshi wa Uganda karibu na mpaka na DRC kufuatia vita na waasi wa ADF mwezi Machi 2007.
Wanajeshi wa Uganda karibu na mpaka na DRC kufuatia vita na waasi wa ADF mwezi Machi 2007. Photo: AFP Photo/Peter Busomoke
Matangazo ya kibiashara

ADF ambayo ilitangazwa na kundi la Islamic State (EI) kama tawi lake katika Afrika ya Kati (Iscap kwa Kiingereza), inatuhumiwa kwa mauaji ya maelfu ya raia nchini DRC na kufanya mashambulizi nchini Uganda, mashambulizi ya hivi karibuni katika mji mkuu wa Kampala nchini humo ya mwezi Oktoba na Novemba 2021.

Tangu mwisho wa mwezi Novemba 2021, majeshi ya DRC na Uganda yamekuwa yakifanya operesheni za pamoja kujaribu kuwazuia. Kati ya 20 na 30 "Wapiganaji wa ADF walivuka mpaka na kingia nchini Uganda, jana usiku katika mto Semliki", kwenye mpaka kati ya DRC na Uganda, msemaji wa jeshi la Uganda Félix Kulayigye aliandika katika taarifa kwa vyombo vya habari.

"Huduma zetu za kijasusi zilifaulu na zilinaswa," aliendelea, akisema kuwa wanachama kumi na moja wa ADF waliuawa na wengine wanane kukamatwa. Mwanajeshi mmoja pia aliuawa katika mapigano hayo, ambayo "bado yalikuwa yakiendelea" Jumanne asubuhi, kulingana na Bw Kulayigye.

Wakichukuliwa kuwa ndio walioua zaidi kati ya makundi mia moja yenye silaha yaliyopo mashariki mwa DRC kwa zaidi ya miaka 25, waasi wa ADF wamekuwa wakishambulia raia na maeneo ya jeshi la DRC tangu mwaka 2014 katika eneo la Beni, ambako wamekita mizizi kwenye mpaka na Uganda.

Pia wanashutumiwa na Kampala kwa kuhusika na mashambulizi ya hivi majuzi katika ardhi yake mnamo mwezi Oktoba na Novemba 2021, ambayo yalisababisha vifo vya watu 5 na kujeruhi watu kadhaa. Mnamo 2021, Marekani ililiweka kundi la waasi la ADF kwenye orodha ya makundi ya 'kigaidi'.

Mamlaka ya Uganda pia iliwanyooshea kidole ADF mnamo Agosti 2021, baada ya shambulio la bomu lililoshindwa wakati wa mazishi ya kamanda wa jeshi, Paul Lokech, aliyepewa jina la utani la "Simba wa Mogadishu" kwa kuongoza mashambulizi dhidi ya Waislam wa Al Shabab nchini Somalia ndani ya kikosi cha AMISOM, jeshi la Umoja wa Afrika nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.