Pata taarifa kuu
KENYA-USHIRIKIANO

Kenya yasitisha safari za ndege na Dubai

Nchini Kenya, Mamlaka ya Usafiri wa Anga imetangaza Jumanne hii, Januari 11, 2022, kusitisha safari zote za ndege za abiria kutoka Dubai. Hatua hii ni ya ulipizaji kisasi wakati tangu mwisho wa mwezi wa Desemba, Umoja wa Falme za Kiarabu umesitisha kwa muda safari za ndege za abiria kutoka Kenya kutokana na tuhuma za biashara haramu za vipimo vya uongo vya Covid.

Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.
Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. YASUYOSHI CHIBA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Usitishwaji huo ulianza usiku wa manane Jumatatu, kulingana na mkurugenzi mkuu wa shirika la ndege la Kenya na utadumu kwa siku saba. Hatua hii inahusu ndege zote za abiria kutoka Umoja wa Falme za Kiarabu, ikiwa ni pamoja na safari zinazoendelea katika mataifa mengine, kwa ndege zinazotua nchini humo. Hata hivyo, haijumuishi safari za ndege za mizigo, ambazo ni za kawaida sana kati ya nchi hizo mbili.

Mamlaka ya Kenya haifanyi siri jambo hilo, ni hatua ya "kuridhiana", ili kuepuka kusema kuwa ni "ulipizaji kisasi". Wiki iliyopita Umoja wa Falme za Kiarabu ulirejelea upya hatua yake ya usitishaji wake wa safari zote za ndege kutoka Kenya, kwa muda wa wiki tatu sasa. Hatua ambayo iimeikera Nairobi.

Dubai inatetea hatua yake kwa kusema kuwa nchini Kenya visa vya maambukizi ya Covid-19 vimeongezeka.

Uchumi wa Kenya umeathirika pakubwa kutokana na vikwazo vya kusafiri kote ulimwenguni tangu kuanza kwa janga hili na mara kwa mara Imepinga hatua za upande mmoja kuhusu ufikiaji wa Kenya zilizowekwa bila mashauriano na nchi mbalimbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.