Pata taarifa kuu
Sierra Leone-Liberia

Charles Taylor akutwa na hatia ya uhalifu wa kivita ulitekelezwa nchini Sierra Leone

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor anaeshutumiwa makosa ya uhalifu wa kivita yaliofanyika nchini Sierra Leone, amekutwa na hatia na mahakama maalumu ya uhalifu wa kivita nchini Sierra Leone ilioko The Heuge nchini Uholanzi, baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo kwaki pindi cha miaka mitano. Hii ni mara ya kwanza mahakama ya kimataifa inatowa hukumu dhidi ya rais wa zamani. 

Kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor mahakamani
Kiongozi wa zamani wa Liberia Charles Taylor mahakamani TV5
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi wa zamani wa Uasi ambae baadae alitokea kuwa rais wa Liberia kupitia uchaguzi mkuu charles Taylor mwenye umri wa miaka 64 hatma yake imetatambulika leo alhamisi baada ya kukutwa na makosa ya uhalifi wa kivita.Anashutumiwa kuunga mkono kundi la waasi wa Sierra Leone la RUF na kuhusishwa katika mtandao wabiashara haramu ya silaha na alimasi. Anashutumiwa pia kosa la kufadhili kundi hilo la uasi  kwa lengo la kuendelea kujizolea alimasi katika kipindi cha vita iliopelekea watu laki moja na elfu ishirini kupoteza maisha kati ya mwaka 1991-2001.

Kabla ya kuwa kiongozi wa kundi la Uasi, Charles Taylor aliishi katika maeneo ya kitajiri yenye asili ya Afrika na Marekani. Alisoma chuo kikuu nchini Marekani na baadae kuhudumu katika wizara mbalimbali nchini Liberia na baadae kuhusika katika vitendo vya ulaji rushwa vilivyo mfikisha gerezani mwaka 1983 baada ya kupitisha mlango wa nyuma takriban dola za kimarekani laki tisa na alikimbilia nchini Marekani ambako alikamatwa baadae.

Alifaulu kutoroka jela kwa msaada wa shirika la kijasusu la Marekani CIA na kukimbilia nchini Côte d’Ivoire na baadae alielekea kupata mafunzo ya kijeshi katika kambi moja nchini Liberia

katika usiku wa kuamkia sikuu ya kuzaliwa Yesu Christo mwaka 1989, Charles Taylor alianzisha vita kubwa kuwahi kutokea barani Afrika na kundi la NPFL ambapo aliajiri watoto wadogo katika jeshi lake waliotumia dawa za kulevya na kuhusika katika vitendo mbalimbali vya kikatili vikiwemo ubakaji, mauaji ya kinyama na hata vitendo vya kula nyama za binadamu.

Katika mwaka 1997 baada ya mkataba wa amani, Charles Taylor alichaguliwa kuwa rais kupitia uchaguzi mkuu

Mnamo mwaka 1999 uasi ulianza tena upya na kundi la wananchi wa Liberia waliojiunga pamoja kwa ajili ya maridhiano na demokrasia (LURD) kaskazini mwa Liberia ulioishia jijini Monrovia. Baada ya shinikizo kutoka jamii ya kimataifa na kuhusishwa katika uungwaji mkono wa kundi la RUF nchini Sierra Leone, Chrles Taylor  alikubali kupewa hifadhi nchini Nigeria mwaka 2003. Hapo alifkiri kukimbia mkono wa sheria.

Mwaka 2006, alikamatwa na kupelekwa moja kwa moja kwenye mahakama maalum kuhusu uhalifu wa kivita uliotendeka nchini Sierra Leone.

yaliofanyika nchini Sierra Leone, yalitendeka pia nchini Liberia

Kwa hali yoyote itayo tokea kuhusu hukumu ya kiongozi huyo, wananchi wa liberia wataendelea kusikitishwa kuona rais wao huyo wa zamani kutoadhibiwa kufuatia mauaji alioyatekeleza nchini Liberia..

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.