Pata taarifa kuu

Macron-Maduro wazungumza katika mkutano wa COP27, kulikoni

Marais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Rais wa Venezuela Nicolas Maduro walikuwa na mazungumzo mafupi na muhimu Jumatatu, Novemba 8 kando ya mkutano wa kilele kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP27) huko Sharm el-Sheikh, Misri. 

Mkutano kati ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Nicolas Maduro, kando ya mkutano wa kilele kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP27) huko Sharm-el-Sheikh, Jumatatu Novemba 7, 2022.
Mkutano kati ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Nicolas Maduro, kando ya mkutano wa kilele kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP27) huko Sharm-el-Sheikh, Jumatatu Novemba 7, 2022. via REUTERS - MIRAFLORES PALACE
Matangazo ya kibiashara

Video ya mkutano huu ilitolewa na ikulu ya rais wa Venezuela. Mkutano huu unaonekana kuwa ni muhimu zaidi kwani Ufaransa bado haimtambui rasmi Nicolas Maduro kama Rais wa Venezuela.

Je, huu ni mwanzo wa kurjeswa kwa mahusiano kati ya Paris na Caracas? Ni kando ya mkutano wa kilele kuhusu mabadiliko ya tabianchi (COP27) ambapo marais hao wawili walikutana. Mazungumzo yao yalidumu kwa dakika mbili tu. Rais wa Ufaransa anakwepa swali la mwenzake wa Venezuela, lakini anamfahamisha kwamba angefurahi kuzungumza naye zaidi kwenye simu.

Katika mazungumzo hayo, Emmanuel Macron alimwita Nicolas Maduro "rais". Jambo ambalo linashangaza, kwa sababu Ufaransa haimtambui rasmi Nicolas Maduro kama raishalali wa Venezuela. Kama Marekani, Ufaransa bado inamuunga mkono kiongozi wa upinzani Juan Guaido kama rais wa mpito, ingawa rais huyo amepoteza nguvu zake nyingi za kisiasa.

Mabadiliko mapana ya kidiplomasia?

Hatua ya Emmanuel Macron dhidi ya yule anayechukuliwa kama mtu aliyetengwa ni sehemu ya mabadiliko makubwa ya kidiplomasia. Mnamo 2019, Marekai iliweka msururu wa vikwazo dhidi ya Venezuela, pamoja na vikwazo vya mafuta. Lakini kutokana na kupanda kwa bei ya nishati kufuatia vita vya Ukraine, Washington ilipunguza baadhi ya vikwazo hivyo.

Rais wa Ufaransa alisema Juni mwaka jana kwamba rasilimali zinapaswa kutafutwa mahali pengine na kwamba mafuta ya Venezuela lazima yarudishwe sokoni. Maneno yaliyothaminiwa na Nicolas Maduro ambaye, Jumatatu hii, Novemba 7, hakuficha kuridhika kwake kwa kuweza kuzungumza kwa maneno machache na Emmanuel Macron.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.