Pata taarifa kuu

Mkutano mkubwa wa Mabadiliko ya Tabia nchi wa Umoja wa Mataifa wafunguliwa Sharm el-Sheikh

Mkutano wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa Kimataifa wa tabianchi COP27 mwaka huu unafanyika huko Sharm el-Sheikh,nchini Misri wakati ambapo dunia inashuhudia ongezeko la hali mbaya ya hewa duniani kote, shida ya nishati iliyochochewa na vita vya Ukraine, na takwimu za wanasayansi zinasisitiza kwamba ulimwengu haufanyi vya kutosha kukabiliana na utoaji wa hewa ya kaboni na kulinda mustakabali wa sayari yetu.

Bango lililoandikwa COP27 kwenye barabara inayoelekea eneo la mkutano katika mji wa mwambao wa Misri wa Sharm el-Sheikh.
Bango lililoandikwa COP27 kwenye barabara inayoelekea eneo la mkutano katika mji wa mwambao wa Misri wa Sharm el-Sheikh. REUTERS - SAYED SHEASHA
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya wawakilishi wa nchi 200 duniani wanakusanyika kwenye mji huo kujaribu kwa mara nyingine kutafuta majibu ya jinsi ya kushughulikia taathira za Mabadiliko ya Tabianchi katika wakati ulimwengu unakabiliwa na vita na mzozo mkubwa wa kiuchumi.

Wakuu wa nchi, serikali, mawaziri, wasuluhishi pamoja na wanaharakati wa tabianchi, mameya, wawakilishi wa mashirika ya kiraia, watendaji wa kuu wa kampuni wanakutana katika mji wa pwani ya Misri, Sharm el-Sheikh katika mkutano mkubwa kuhusu tabia nchi.

Jana Jumamosi Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliwahimiza viongozi watakaohudhuria mkutano huo kuuweka ulimwengu katika njia sahihi ya kupunguza gesi zinazochafua mazingira na kutimiza ahadi zao za ufadhili kusaidia nchi maskini kuelekea matumizi ya nishati safi.

Mkutano huo wa 27 wa nchi wanachama wa mkataba wa mabadiliko ya tabia nchi, UNFCCC, COP27 utasongesha yale yaliyokubaliwa kwenye CO26 na kutoa hatua zinazoendana na kutatua dharura ya tabia nchi – kuanzia kupunguza hewa chafuzi, kutekeleza ahadi za kufadhili hatua kwa tabia nchi katika nchi zinazoendelea.

Tangu mwaka 1994, wakati mkataba huo ulipoanza kutekelezwa, kila mwaka Umoja wa Mataifa umekuwa ukiwaleta pamoja karibu kila nchi zote duniani kwa ajili ya mikutano ya kimataifa ya tabianchi au “COPs”, ambayo ni kifupi cha “Mkutano wa nchi wanachama”.

COP27 inasaka kurejesha tena mshikamano kati ya mataifa na kutekeleza Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi kwa ajili ya wakazi wa dunia na sayari dunia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.