Pata taarifa kuu

Kabla ya COP27, Misri yakabiliwa na changamoto za ushiriki na haki za binadamu

Mwezi mmoja kabla ya mkutano kuhusu Tabia nchi (COP27), Misri inaongeza wito wake kwa viongozi wa dunia kufanya mkutano huu wa kilele kuhusu Tabia nchi kuwa mkutano wa kidiplomasia usioweza kupingwa, huku ikijaribu kuepuka ukosoaji wa ukiukaji wake wa haki za binadamu.

Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi katika mkutano wa kilele wa nchi za Kiarabu huko Sharm el-Sheikh, Misri, Machi 29, 2015.
Rais wa Misri Abdel Fattah el-Sisi katika mkutano wa kilele wa nchi za Kiarabu huko Sharm el-Sheikh, Misri, Machi 29, 2015. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa, hakuna mkuu wa nchi ambaye amethibitisha rasmi kushiriki katika mkutano huo ambao utafunguliwa mnamo Novemba 6 huko Sharm el-Sheikh kwenye Bahari Nyekundu, lakini kutokuwepo tayari kumeonekana: Mfalme Charles III hatakuwepo.

Rais wa COP27, mkuu wa diplomasia ya Misri Sameh Choukri, "amekatishwa tamaa", kulingana na afisa wa Misri aliyenukuliwa na gazeti la kila siku la Uingereza la The Guardian. "Tunatumai hii haiashirii kuwa Uingereza inarudi nyuma kutoka kwa harakati za kimataifa juu ya mabadiliko ya Tabia nchia," ameongeza.

Na hii ni wakati ambapo dunia tayari imeshikiliwa na masuala mengine muhimu kama vile uvamizi wa Urusi nchini Ukraine au kupanda kwa bei za vyakula na nishati. Hata hivyo, Cairo inataka kwanza kuhamasisha nchi zilizoendelea kiviwanda na zinazochafua mazingira kushiriki mkutano huu utakaofanyika barani Afrika.

Jumuiya ya kimataifa inaendelea kuthibitisha tena lengo la Mkataba wa Paris wa kudhibiti ongezeko la joto duniani hadi nyuzi joto 1,5°C juu ya viwango vya kabla ya kuanza kwa viwanda - ambalo linaonekana kutoweza kufikiwa kwa sasa, kwa kuwa tayari tuko karibu na nyuzi joto 1.2°C. Kiwango ambacho athari za ongezeko la joto duniani tayari zinaongezeka duniani kote - ukame, mafuriko, mawimbi ya joto, moto mkubwa - unaoathiri hasa nchi maskini zaidi, ambazo zinawajibika kwa uzalishaji wa gesi chafu zinazotokana na ongezeko la joto duniani.

Kwa hivyo nchi hizi zinadai ufadhili maalum kufidia "hasara na uharibifu" uliopatikana, suala ambalo linatazamiwa kujadiliwa vikali katika mkutano huo, matajiri zaidi, mara nyingi wachafuzi wakubwa, wakisitasita sana. Mjadala huo unafanyika katika hali ya kutoaminiana, kwani nchi tajiri bado hazijatimiza ahadi yao ya kusaidia nchi maskini kwa dola bilioni 100 kwa mwaka kwa ajili ya kupunguza uzalishaji na kukabiliana na hali hiyo.

Mahmoud Mohieldin, afisa mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Tabia nchi, hata hivyo amekaribisha "ahadi ya nchi kadhaa kutimiza sehemu yao ya ahadi ya Copenhagen ya kutoa dola bilioni 100 kwa mwaka" hata kama kiasi hiki "hakiwakilisha 3% tu ya mahitaji". Lakini kwa upande wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, anasema "ahadi za pamoja za serikali za G20 ni dhaifu sana na zimechelewa sana".

Nchini Misri, Waziri wa Mazingira Yasmina Fouad hivi karibuni alikiri, wasiwasi wa mazingira kwa muda mrefu umezingatiwa "anasa" ambayo nchi ya watu milioni 104 haikuweza kumudu. Leo, imejiwekea lengo la kufikia 42% ya umeme wake kutoka kwa nishati mbadala ifikapo 2035 lakini kwa wahifadhi, hii haitoshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.