Pata taarifa kuu

COP: Majadiliano juu ya mabadiliko ya Tabia nchi katika nchi maskini kufanyika Kinshasa

Mwezi mmoja kabla ya mkutano kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi (COP27) huko Sharm el-Sheikh, Misri, DRC inaandaa Jumatatu hii, Oktoba 3 na kwa siku tatu mzungumzo kabla ya mkutano kuhusu Tabia nchi (COP) huko Kinshasa. 

Nchini DRC, misitu inatishiwa na kilimo na uchimbaji wa mkaa, lakini pia na miradi ya mafuta, ambayo mamlaka ya DRC ilitoa wito wa kutolewa kwa zabuni mwezi Julaimwaka huu. Hapa, Hifadhi ya Kitaifa ya Kahuzi Biega mashariki mwa DRC.
Nchini DRC, misitu inatishiwa na kilimo na uchimbaji wa mkaa, lakini pia na miradi ya mafuta, ambayo mamlaka ya DRC ilitoa wito wa kutolewa kwa zabuni mwezi Julaimwaka huu. Hapa, Hifadhi ya Kitaifa ya Kahuzi Biega mashariki mwa DRC. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Takriban mawaziri 80 wa mazingira kutoka duniani kote wanatarajiwa katika mji mkuu wa DRC kujiandaa kwa mazungumzo kuhusu Tabia nchi.

"Mazungumzo haya ya kabla ya mkutano kuhusu Tabia nchi hayana mwelekeo wa kisheria. Huu sio mkutano rasmi wa mazungumzo. Ni mkutano, bila shaka, rasmi, lakini wakati ambao nakala ya mazungumzo hayatafunguliwa tena. Mkutano muhimu utafanyika kwa wiki ya pili ya mazungumzo huko Sharm el-Sheikh”, ameelezea Balozi Tosi Mpanu Mpanu, kiongozi wa ujumbe wa DRC kuhusiana na Mkataba wa Tabia nchi, kwa sababu unaweza kuzaa matunda, amebaini Claire Fages, wa kitengo cha RFI katika kanda ya Afrika.

Hakuna nakala ya kisheria ya kusubiri, kwa hivyo, kutoka kwa mkutano huu wa kabla ya mkutano kuhsu Tabia nchi huko Kinshasa, lakini majadiliano yasiyo rasmi kati ya mawaziri yanaweza kuzaa matunda, baadhi ya wajumbe katika mazungumzo hayo wana matumaini. Hasa kwenye kile kinachojulikana kama ripoti ya hasara na uharibifu ambao tayari umesababishwa na mabadiliko ya Tabia nchi kwa nchi maskini.

Haki ya kutoa gesi chafu

DRC, nchi mwenyeji wa mkutano wa kabla mkutano kuhusu Tabia nchi, inachukua fursa hiyo kujionyesha kama nchi ya suluhisho, ambayo inahitaji ufadhili wa kuhifadhi misitu yake, mifereji ya kaboni kwa sayari nzima. Misitu hii inatishiwa na kilimo na uchimbaji wa mkaa, lakini pia, na miradi ya mafuta, ambayo mamlaka ya DRC ilizindua wito wa zabuni mwezi Julai mwaka huu, shirika la kimataifa linalohusika na masuala ya mazingira Greenpeace barani Afrika limebaini.

Vigingi hivyo vinajulikana kwa DRC, anaripoti mwandishi wetu wa Kinshasa, Patient Ligodi. Nchi inatetea haki yake ya kutoa gesi chafuzi kwa ajili ya maisha ya watu wake, mamlaka inasema. Akizungumza na wajumbe hao, Waziri Mkuu, Jean-Michel Sama Lukonde, aliomba kupitishwa kwa msimamo wa pamoja wa kimataifa kuhusu hali ya dharura. Ametetea matamshi yake kwa ukweli kwamba baadhi ya nchi za Ulaya zimerejea kwenye matumizi ya vyanzo vya nishati chafuzi ambavyo walikuwa wamevipiga marufuku hapo awali ili kuepusha matokeo ya upungufu wa nishati waliyowekewa na vita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.