Pata taarifa kuu

Umoja wa Mataifa walaani 'unyanyapaa' wa walinda amani wake nchini DRC

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ameshutumu siku ya Ijumaa mbele ya Baraza la Usalama ghasia za hivi majuzi dhidi ya tume ya Umoja wa Mataifa nchini humo, zinazolengwa na "udanganyifu na unyanyapaa".

Wanajershi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, walitumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Machi 29, 2022.
Wanajershi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa, MONUSCO, walitumwa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Machi 29, 2022. REUTERS - DJAFFAR SABITI
Matangazo ya kibiashara

"Katika kipindi cha miezi michache iliyopita, kutokana na kuibuka upya kwa kundi la waasi la M23, ujumbe wa Umoja wa Mataifa umepoteza imani kwa wakazi wa mashariki mwa DRC," Bintou Keita mkuu wa ujumbe huu wa kulinda amani wa MONUSCO amesema.

"Hali hii ilizusha vurugu na unyanyapaa dhidi ya MONUSCO, na kusababisha maandamano mapya yenye vurugu na matukio makubwa na kusababisha vifo vya waandamanaji kadhaa na wafanyakazi wanne wa tume hiyo," ameongeza, akilaani vikali "vitendo vya kuchochea chuki, uhasama na vurugu. ".

Mwishoni mwa mwezi wa Julai, waandamanaji wenye hasira walivamia na kupora majengo ya MONUSCO. Ujumbe huo, moja ya jumbe kubwa zaidi katika Umoja wa Mataifa duniani ukiwa na askari wapatao 14,000, unashutumiwa kwa kutofaulu katika vita dhidi ya makundi yenye silaha.

"Kufuatia matukio haya, Rais wa DRC, Felix Tshisekedi ameiagiza serikali yake kutathmini upya mpango wa mpito ili kuharakisha kuondoka kwa MONUSCO. Tumejipanga kikamilifu kufanya kazi kwa karibu na serikali kufikia malengo haya" , amesema Bintou Keita.

Mkuu wa MONUSCO pia ameelezea wasiwasi wake kwamba "makundi yenye silaha yanaendelea kuwa tishio kubwa na kufanya vurugu dhidi ya raia" mashariki mwa nchi, akitoa mfano wa kundi la M23 na wanamgambo wa Codeco ( Ushirika wa Maendeleo ya Kongo) na Mai-Mai.

"Ukosefu huu wa usalama unachochea ukiukwaji wa haki za binadamu na umezidisha hali mbaya ya kibinadamu," amesema, akibainisha kuwa watu milioni 27 wanahitaji msaada wa kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.