Pata taarifa kuu

UN: Nchi haziwajibiki kuzuia ongezeko la joto duniani

Ripoti mpya ya umoja wa Mataifa, inasema kuwa ahadi ya Jumuiya ya kimataifa kuhusu kudhibiti ongezeko la joto kwa nyuzi 1.5 bado haikaribiwi ripoti inayotolewa ikiwa ni chini ya wiki mbili kabla ya kufanyika kwa majadiliano kuhusu hali ya joto duniani.

Umoja wa Mataifa waonya kuhusu nchi kushindwa kutimiza ahadi ya kuzuia ongezeko la joto kwa nyuzi 1.5.
Umoja wa Mataifa waonya kuhusu nchi kushindwa kutimiza ahadi ya kuzuia ongezeko la joto kwa nyuzi 1.5. AP - Alberto Pezzali
Matangazo ya kibiashara

Ripoti hiyo imeongeza kuwa, ahadi zote zilizotolewa kwa pamoja na zaidi ya mataifa 190, ambazo zilipelekea kutiwa saini kwa mkataba wa Paris kuhusu mabadiliko ya tabia nchi mwaka 2015 huenda zisitekelezeke.

 

Wakati huu sayari ya dunia ikishuhudia athari kubwa za mabadiliko ya hali ya hewa kutokana na ongezeko la joto, vimbunga na mafuriko baada tu ya kufikia nyuzi joto 1.2, wataalamu wanasema nchi bado zinashindwa kuchukua hatua stahiki kudhibiti gesi Hamijoto.

 

Kwa mujibu wa mkurugenzi wa taasisi ya umoja wa mataifa kuhusu hali ya hewa, Simon Stiell, malengo yaliyowekwa na dunia hayajakaribiwa hata kidogo jambao ambalo itakuwa ngumu kuwa na udhibiti wa nyuzi joto 1.5.

 

Kati ya nchi 193, ni mataifa 24 pekee ambayo yamerekebisha mipango yao kutokana na makubaliano ya mkutano wa mwaka uliopita mjini Glascow, Scotland.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.