Marekani: watu wasiopungua 44 wapoteza maisha kutokana na hali mbaya ya hewa
Vimbunga, mafuriko ya ghafla na theluji vimesababisha vifo vya watu wasiopungua 44 nchini Marekani tangu Jumamosi.
Imechapishwa:
Hali hiyo imevuruga safari za ndege na shughuli zimezorota katika sekta ya uchukuzi wa magari katika kipindi hiki cha harakati kubwa kwa ajili ya siku kuu za mwisho wa mwaka.
Vimbunga vilipiga katika jimbo la Texas (kusini) mwishoni mwa wiki iliyopita na kuendelea Jumatatu wiki hii ikiwa ni pamoja na dhoruba kali za blizzard, mvua na mafuriko katika sehemu kubwa ya Marekani.
Mamilioni ya raia walikuwa wamekwama katika viwanja vya ndege Jumatatu hii baada ya safari 2,100 za ndege zilifutwa na zingine 3700 zikicheleweshwa, kulingana na mtandao wa shirika la ndege la FlightAware.
Hali mbaya ya hewa ilisababisha pia safari 1,640 za ndege kufutwa na zaidi 6,400 kucheleweshwa Jumapili, hasa kwa sababu ya mifumo ya dhoruba inayopiga kambi juu ya anga la jimbo la Texas.
Jumatatuhii jimbo la Chicago limekumbwa na hali mbaya ya hewa, ambapo kumeshuhudiwa dhoruba, vimbunga, mvua kali na mafuriko. Upepo mkali ulisababisha ndege 1,200 kukwama kwenye viwanja mbalimbali vya ndege.
Katika jimbo pekee la Texas watu 11 wamepoteza maisha kutokana na hali hiyo mbaya ya hewa.