Pata taarifa kuu
PAKISTAN-MAPOROMOKO-USALAMA

Kiwanda chaporomoka Pakistan: watu 16 wapoteza maisha

Watu kumi na sita wamepoteza maisha na mamia wengine wamenaswa katika vifusi wakati kiwanda cha mifuko ya plastiki kiliporomoka Jumanne wiki hii karibu na mji wa Lahore mashariki mwa Pakistan.

Waokoaji wa Pakistan wakibeba waathirika wa maporomoko ya kiwanda katika eneo la viwanda la Lahore, Novemba 4, 2015.
Waokoaji wa Pakistan wakibeba waathirika wa maporomoko ya kiwanda katika eneo la viwanda la Lahore, Novemba 4, 2015. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

" Maafisa wa Idara ya huduma za dharura waliiondoa miili kumi na sita ya watu waliopoteza maisha, na watu 40 walioruhiwa walmeelekwa hospitali ", mkuu wa huduma za utawala wa mji, Muhammad Usman amebaini.

Watu mia moja walikuwa bado wakiwa katika jengo, msemaji wa huduma za dharura, Jam Sajjad Hussain, amesema, huku akiongeza kuwa maafisa wa Idara hiyo kutoka wilaya za jirani wameitwa ili kuja kusaidia.

Tukio hilo baya kabisa limetokea katika kiwanda cha kutengeneza mifuko ya plastiki ya polyethilini cha gorofa tatu, katika eneo la viwanda la Sundar, kilomita 45 kutoka katikati mwa mi wa Lahore.

Tukio hili linakuja siku chache tu baada ya tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 390 nchini Pakistan na Afghanistan, na kuharibu maelfu ya majengo.

Wafanyakazi wengi wa kiwanda hicho wameihakikishia runinga mbalimbali kwamba nyufa zilitokea katika kiwanda hicho wakati wa tetemeko la ardhi, na mmiliki aliendelea na ujenzi wa ghorofa ya nne licha ya hali hiyo kujitokeza.

Mwaka uliopita Msikiti mmoja uliporomoka katika mji huo, na kuua watu 24. Na watu zaidi ya 200 waliuawa katika maporomoka mbalimbali ya majengo katika mfululizo wa mvua kubwa zilizonyesha pamoja na mafuriko mwaka 2014.

Septemba 11, 2012, wafanyakazi 255 walikufa katika tukio la moto wa kiwanda cha nguo katika mji wa bandari wa Karachi, moja ya tukio baya ya viwanda katika historia ya Pakistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.