Pata taarifa kuu

Serikali ya Mali inakataza vyombo vya habari kuchapisha shughuli za vyama vya siasa

Mamlaka ya Mali inayotawaliwa na jeshi siku ya Alhamisi imepiga marufuku vyombo vya habari kutochapisha shughuli za vyama vya siasa, baada ya kusimamisha shughuli hizo siku moja kabla.

Assimi Goita, Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Mali.
Assimi Goita, Mkuu wa utawala wa kijeshi nchini Mali. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Kufuatia kusitishwa kwa shughuli za vyama vya siasa, Mamlaka Kuu ya Mawasiliano "inavitaka vyombo vyote vya habari (redio, televisheni, magazeti na magazeti ya mtandaoni) kusitisha utangazaji na uchapishaji wa shughuli za vyama vya siasa na shughuli za sera ya chama," chombo hiki kimesema katika taarifa kwa vyombo vya habari. HAC haielezi ni vyombo gani vya habari vinavyokiuka vitakabiliwa na sheria kali.

Siku ya Jumatano utawala wa kijeshi uliagiza kusitiishwa "hadi uamuzi mwingine utapochukulia "shughuli za mashirika na vyama vya kisiasa, kutokana na "majadiliano tasa" na "upotoshaji". Hivi ni vikwazo vipya kwa usemi wowote wa upinzani au upinzani wa dhidi ya wanajeshi ambao walichukua madaraka kwa nguvu mnamo Agosti 2020 kwa kumpindua rais wa kiraia Ibrahim Boubacar Keïta.

Vikwazo hivi vipya vinakuja wakati jeshi limeshindwa katika ahadi yake, iliyotolewa chini ya shinikizo la Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS), kukabidhi madaraka kwa raia ifikapo Machi 26, 2024. Mali imetumbukia katika mgogoro mkubwa mkubwa wa pande nyingi tangu 2012.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.