Pata taarifa kuu

Mali: Utawala wa kijeshi wasitisha shughuli za mashirika na vyama vya siasa

Kanali Abdoulaye Maïga, Waziri wa Mambo ya Ndani na msemaji wa serikali ambaye ametangaza habari siku ya Jumatano usiku, amehalalisha uamuzi huu kwa sababu za kisiasa na kiusalama.

Abdoulaye Maïga, msemaji wa utawala wa kijeshi. Picha ya kumbukumbu ya Julai 31, 2023.
Abdoulaye Maïga, msemaji wa utawala wa kijeshi. Picha ya kumbukumbu ya Julai 31, 2023. AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu wa kikanda, Serge Daniel

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Kanali Abdoulaye Maïga, Waziri wa Utawala wa Wilaya na msemaji wa serikali, ameeleza kuwa hali ya usalama katika maeneo mbalimbali ni moja ya sababu za kusimamishwa shughuli za mashirika na vyamavya siasa nchni Malihadi itakapochukuliwa uamuzi mwingine . "Shughuli za mashirika na vyama vya kisiasa nchini kote zimesimamishwa hadi itakapotangazwa uamuzi mwingine, kwa sababu za usalama wa taifa," inasema agizo lililotolewa katika baraza la mawaziri na mkuu wa mkuu wa utawala wa kijeshi, Kanali Assimi Goïta, na kusomwa mbele ya waandishi wa habari na Kanali Maïga.

Kanali Maïga ameeleza kuwa kurejeshwa kwa mji wa Kidal, mnamo mwezi wa Novemba 2023, kutoka mikononi mwa waasi wa zamani pamoja na maeneo mengine hakumaanishi mwisho wa ugaidi au masuala ya usalama. Ameongeza kuna changamoto nyingine za kiusalama kukabiliwa, wakati huo huo, wanasiasa wa Mali wanaongoza "mijadala tasa" na wanashtumiwa kutaka kuchangia katika kuzorota kwa usalama.

Waziri huyo amerejelea sauti nyingi za kisiasa za ndani zinazozidi kusikika ambazo zinathibitisha kuwa kipindi cha mpito kimemalizika tangu Machi 26. Na kunahitajika kurejea kwa haraka kwa utaratibu wa kikatiba.

Utawala wa kijeshi wa Mali inapuuzilia mbali hoja hii na kuweka mbele sababu nyingine ya kuhalalisha kipimo cha kusimamishwa kwa shughuli za mashirika na vyama vya siasa: haja, kwa mujibu wake, kuweka mazingira ya utulivu wakati ambapo mazungumzo ya kitaifa kati ya wadau nchini Mali yametangazwa kushughulikia matatizo ya nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.