Pata taarifa kuu
USALAMA-JAMII

Raia watatu wajeruhiwa baada ya jeshi la Mali na Wagner kuvamia Mauritania

Wanajeshi kutoka jeshi la Mali na mamluki wa Urusi kutoka kundi la Wagner waliingia katika eneo la Mauritania Jumapili Aprili 7. Uvamizi huo ulifanyika kama sehemu ya oparesheni ya kupambana na ugaidi ambayo si Bamako wala Nouakchott wametoa taarifa rasmi lakini wakati huo, kwa mujibu wa taarifa kutoka RFI, raia watatu walijeruhiwa kwa risasi. Tukio hili lilitokea katika kijiji cha Madallah, karibu na Fassala, Wilaya du Hodh El Chargui, kusini-mashariki mwa Mauritania.

Askari wa Kikosi cha Wanajeshi wa Mali huko Timbuktu, Septemba 9, 2021.
Askari wa Kikosi cha Wanajeshi wa Mali huko Timbuktu, Septemba 9, 2021. AFP - MAIMOUNA MORO
Matangazo ya kibiashara

Walikuwa wanatafuta wanajihadi kutoka Katiba Macina ya Jnim (Kundi linalodai Kutetea Uislamu na Waislamu), lenye mafungamano na Al-Qaeda. Kulingana na vyanzo vya ndani - maafisa waliochaguliwa, wakaazi na wataalamu wa usalama - waliohojiwa na RFI, wanajeshi wa Mali na wasaidizi wao wa Urusi kutoka Wagner walivuka mpaka wa Mauritania kabla ya saa nne asubuhi. Kisha wakaingia katika kijiji cha Madallah na kufyatua risasi.

Vijana watatu waliokuwa wakiendesha pikipiki walijeruhiwa. Nyumba pia ziliharibiwa na risasi. Watu wanne walikamatwa na kuhojiwa na wanajeshi wa Mali na wasaidizi wao Wagner, kabla ya kuachiliwa.

Askari wa Mauritania kisha walikwenda katika kijiji cha Madallah ili kujaribu kuwatuliza wakazi na kuwashauri kuepuka kusafiri katika eneo hili hatari la mpaka.

"Sio kosa, walikuwa wakiwafuata magaidi," kinathibitisha chanzo cha usalama cha Mali ambacho kinahakikisha kwamba wanajihadi kadhaa waliuawa wakati wa operesheni hiyo, bila kutaja idadi yao au upande gani wa mpaka. Msitu mkubwa wa Wagadou - eneo la makimbilio la magaidi wa Jnim, upande wa Mali - uko karibu sana.

Matukio yanayohusisha jeshi la Mali na Wagner kwenye mpaka wa Mauritania ni ya mara kwa mara. Miaka miwili iliyopita, tume ya pamoja ya uchunguzi iliundwa hata baada ya vifo vya raia kadhaa wa Mauritania. Kwa ombi la RFI, ubalozi wa Mauritania mjini Bamako haukutoa maoni na Nouakchott haijatoa taarifa rasmi. Kwa upande wa jeshi la Mali, halikutoa maelezo zaidi.

Jeshi pia halikutaka kujibu kuhusu swala la shambulio la ndege zisizo na rubani lililotekelezwa siku ya Jumapili asubuhi karibu na Zorho, takriban kilomita mia moja kaskazini mwa Ber, katika eneo la Timbuktu. Kulingana na vyanzo kadhaa vya usalama na raia, shambulio hili liliua mwanamke na watoto wake wawili. Jeshi halijjatoa taarifa rasmi kuhusu shambulio hili la ndege zisizo na rubani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.