Pata taarifa kuu

Watumishi wa serikali ya kijeshi wameuawa na watu wenye silaha nchini Mali

NAIROBI – Nchini Mali, Mkuu wa wafanyakazi wa uongozi wa kijeshi unaoongozwa na Kanali Assimi Goita  ni miongoni mwa watu wanne waliouawa baada ya msafara wao kushambuliwa na watu wenye silaha siku ya Jumanne wiki hii. 

Wafanyikazi katika serikali ya kijeshi ya Mali wameuawa katika mji wa Nara.
Wafanyikazi katika serikali ya kijeshi ya Mali wameuawa katika mji wa Nara. © Wikimedia/Creative commons
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema Oumar Traore, aliuawa  zaidi ya Kilomita 400 kutoka jiji kuu Bamako, karibu na nchi jirani ya Mauritania, katika eneo linalofahamika kudhibitiwa na makundi ya kijihadi.

Aidha, maelezo kutoka kwenye serikali hiyo ya kijeshi iliyothibitisha mauaji hayo imesema, mazishi ya mkuu huyo wa wafanyakazi inafanyika siku ya Alhamisi kwenye kambi ya jeshi la Kati, karibu na Bamako. 

Inaelezwa kuwa Traore alikuwa amekwenda kuthathmini zoezi la uchimbaji wa visima katika mji wa Nara na msitu wa Wagadou, wakati msafara wao uliposhambuliwa, huku watu wengine walipoteza maisha wakitajwa kuwa mlinzi wake, mkandarasi na dereva. 

Hakuna kundi lilijotokeza kudai kuhusika na mauaji hayo, lakini Mali tangu mwaka 2012, imekuwa ikipambana na utovu wa usalama katika maeneo ya Kaskazini mwa nchi hiyo. 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.