Muungano wa G5 Sahel kwenye njia panda ya kuvunjika
Chad na Mauritania zimeanza mchakato wa kukamilisha kujitoa kwenye muungano wa G5 ulioundwa kwa ajili ya kupambana na makundi ya kijihadi, baada ya nchi nyingine tatu ambazo zilikuwa waasisi kujitoa.
Imechapishwa:
Muungano wa G5 Sahel, uliundwa mwaka 2014, ukijumuisha nchi za Mauritania, Chad, Burkina Faso, Mali na Niger wakisaidiwa na Ufaransa.
Baada ya siku ya Jumamosi, Burkina Faso, Mali na Niger kusema wanajiondoa kutoka kwa muungano huo, Chad na Mauritania wamefungua nafasi ya kuvunja muungano huo.
Mataifa haya yamesema yanaheshimu uamuzi wa kujitawala wa Burkina Faso, Mali na Niger.
Hili linajiri baada ya juma moja lililopita, Burkina Faso, Mali na Niger, kutangaza kuwa wana mpango wa kuunda shirikisho la pamoja kukabiliana na changamoto za usalama, wakati huu pia wakiegemea msaada kutoka Urusi.