Pata taarifa kuu

Mapigano kati ya CSP na Jnim, 'ushindi' kwa mamlaka ya Mali

Nchini Mali, turejelee vita hivi kati ya waasi wa Mfumo wa Kudumu wa Kimkakati (CSP) na wanajihadi wa kundi linalodai kusaidia Uislamu na Waislamu (Jnim) lenye mafungamano na Al-Qaeda vilivyotokea siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita. Vita viliripotiwa karibu na msitu wa Wagadou, kwenye mpaka na Mauritania, na kusababisha, kulingana na vyanzo kadhaa, vifo vya watu kati ya kumi na ishirini katika kambi zote mbili.

Wapiganaji wa CSP mjini Anefis kaskazini mwa Mali mnamo Oktoba 6, 2023.
Wapiganaji wa CSP mjini Anefis kaskazini mwa Mali mnamo Oktoba 6, 2023. © CSP
Matangazo ya kibiashara

Makabiliano haya yanashangaza, kwani CSP na Jnim zote zina kipaumbele cha kupigana na jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Wagner. Jinsi ya kuvielewa vita hivi? Je, ni athari gani kwenye uwanja wa vita?

Kwa mujibu wa mamlaka ya mpito ya Mali ambayo inawashutumu waasi wa CSP na wanajihadi wa Jnim kwa kuunda "chama" cha "kuchochea ugaidi" na "kudhoofisha umoja wa kitaifa na uadilifu wa eneo la Mali" kulingana na masharti ya utaratibu wa pamoja uliozinduliwa mwezi Novemba mwaka jana na vyombo vya sheria vya Mali dhidi ya viongozi kadhaa wa CSP na Jnim, mapigano ya Ijumaa ya wiki iliyopita yanatoa kanusho kubwa.

Udhibiti wa maeneo

Jnim hawakutangaza kuhusu mapigano haya lakini CSP yenyewe ilieleza kuwa lilikuwa ni suala la eneo: wanajihadi wa Jnim wanakataa kwamba CSP, kihistoria iliyopo katika mikoa ya kaskazini, kufanya operesheni za kijeshi kusini mwa Mali.

Aly Tounkara ni mkurugenzi wa Kituo cha Mafunzo ya Usalama na Mikakati katika Sahel (CE3S) huko Bamako anasema "pande hizi mbili husika katika vita hivi wanashindwa kuafikiana kuhusu mbinu za udhibiti na hata utawala wa maeneo," anaelezea mtafiti wa Mali. Malengo hata hivyo yako tofauti, moja likiwa katika mkao wa kuunga mkono uhuru, lingine likiwa katika matumizi madhubuti, ya utekelezaji halisi wa sharia (sheria za Kiislamu. "

"Faida"

CSP na Jnim, hata hivyo, wametangazwa kuwa adui wa pamoja: jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Wagner, ambao wanaonekana kwa kweli kuwa wanufaika wa kwanza wa mgawanyiko huu.

"Ni wazi, mgawanyiko huu unaweza kuchukuliwa na mamlaka ya Mali kama ushindi, anachambua Aly Tounkara, hata kama hii haifai kuwa na athari kwa kiwango cha mbinu, kiutendaji, kama kwa hatua za jeshi la Mali ambazo zinaendelea. "

Kwa wazi, Jeshi la Mali (FAMA) linaweza kunufaika na hili, lakini bila hii kurekebisha mkakati wao wenyewe: "Mradi tu makundi mawili (Jnim na CSP) hayajaunganishwa ndani ya makao makuu sawa na hayashiriki mbinu sawa, athari kwa hatua ya kijeshi (ya FAMA) ni ya chini, ikiwa sio sifuri. » Na kwenye hatua ya CSP, ambayo imeahidi, tangu kushindwa kwake huko Kidal mwezi Novemba mwaka jana, kulipiza kisasi kwa jeshi la Mali na wasaidizi wake wa Wagner?

"Mapigano haya hayabadilishi chochote," anahakikishia mtendaji mkuu wa waasi leo, ambaye anakubali kwamba upinzani wa Jnim unaweza "kupunguza" shughuli zilizopangwa, lakini ambaye anathibitisha kwamba CSP inaendelea kuwa na nia ya kufanya mashambulizi "nchini kote Mali.”

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.