Pata taarifa kuu

Marekani yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Zimbabwe na Rais Mnangagwa

Marekani ilitangaza Jumatatu Machi 4 vikwazo vipya dhidi ya viongozi kadhaa wakuu wa Zimbabwe, akiwemo Rais Emmerson Mnangagwa, wanaotuhumiwa kwa ufisadi na ukiukaji wa haki za binadamu. Hatua hizi mpya - "imara zaidi na zinazolengwa zaidi" - kuchukua nafasi ya mpango mpana, ulizeheka wa miaka 20, dhidi ya Zimbabwe.

Rais wa Zimbabwe bado analengwa na vikwazo vipya vya Marekani. Hapa, Emmerson Mnangagwa (katikati) anahudhuria kikao cha 37 cha kawaida cha Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Februari 17, 2024.
Rais wa Zimbabwe bado analengwa na vikwazo vipya vya Marekani. Hapa, Emmerson Mnangagwa (katikati) anahudhuria kikao cha 37 cha kawaida cha Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa, Februari 17, 2024. © AFP - MICHELE SPATARI
Matangazo ya kibiashara

Kwa jumla, viongozi kumi na moja wakuu wa Zimbabwe, akiwemo Mkuu wa Nchi Emmerson Mnangwaga na mkewe, wanalengwa na vikwazo hivi vipya. Ni pamoja na kuzuiwa mali yoyote nchini Marekani na kupiga marufuku safari zote zisizo rasmi nchini.

Miongoni mwa viongozi wengine waliolengwa: makamu wa kwanza wa rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga, Waziri wa Ulinzi na Masuala ya Maveterani Oppah Muchinguri Kashiri, pamoja na mkuu wa polisi Godwin Matanga.

Kwa mujibu wa Washington, ni suala la kuelekeza upya vikwazo hivi kwenye malengo maalum, ambayo ni "watu muhimu waliohusika na uporaji wa hazina za serikali na ukiukaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wa Zimbabwe", anasema afisa katika Wizara ya Fedha ya Marekani.

Afisa huyu anaongeza kuwa mabadiliko haya yanalenga kufafanua msimamo wa Marekani, yaani kwamba vikwazo hivi haviwalengi raia wa Zimbabwe. Kwa sababu vikwazo vya hapo awali, vilivyowekwa miaka 20 iliyopita na ambavyo vililenga zaidi ya watu sitini na makampuni, vilishutumiwa na serikali, ikizingatiwa kuhusika na hali mbaya ya uchumi nchini.

Rais Emmerson Mnangagwa anakuwa kiongozi wa pili mtawalia wa Zimbabwe kuwekewa vikwazo vya Marekani, baada ya Rais wa zamani Robert Mugabe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.