Pata taarifa kuu

Zimbabwe: Baraza la mawiziri limeunga mkono kusistishwa kwa adhabu ya kifo

Nairobi – Baraza la mawaziri nchini Zimbabwe ,limeunga mkono pendekezo la kuondolewa kwa sheria inayoruhusu adhabu ya kifo, hatua ambayo ni muhimu katika juhudi za kufuta sheria hiyo kwenye taifa hilo la kusini mwa Afrika.

Rais Emmerson Mnangagwa amekuwa akiikashifu sheria hiyo inayopendekeza kifo kwa wahusika ambao uamuzi wa mahakama inawapa hukumu hiyo
Rais Emmerson Mnangagwa amekuwa akiikashifu sheria hiyo inayopendekeza kifo kwa wahusika ambao uamuzi wa mahakama inawapa hukumu hiyo REUTERS - PHILIMON BULAWAYO
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa waziri wa mawasiliano kwenye taifa hilo Jenfan Muswere, uamuzi wa baraza la mawaziri uliafikiwa baada ya kufanyika kwa mashauriano ya kitaifa.

Iwapo bunge litapiga kura kuidhinisha muswada huo, kifungo cha maisha jela kitatumika kama kifungo cha juu zaidi.

Rais Emmerson Mnangagwa amekuwa akiikashifu sheria hiyo inayopendekeza kifo kwa wahusika ambao uamuzi wa mahakama inawapa hukumu hiyo.

Alihukumiwa adhabu ya kifo mwaka wa 1965 kufuatia tuhuma kwamba alihusika na tukio la kulipua treni wakati akipigana dhidi ya utawala wa wazungu nchini humo.

Hukumu ya kifo dhidi ya  Mnangagwa, hata hivyo, ilibadilishwa baada ya mawakili wake kudai kuwa alikuwa na umri mdogo.

Adhabu ya kifo nchini Zimbabwe ni mwendelezo wa sheria ya zama za ukoloni na licha ya kuendelea kutumika kwenye taifa hilo, Harare haijatekeleza mauaji tangu 2005 chini ya sheria hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.