Pata taarifa kuu

Zimbabwe: Mamlaka inaendelea na zoezi la utoaji chanjo dhidi ya kipindupindu

Nairobi – Nchi ya Zimbabwe imezindua zoezi la nyumba kwa nyumba la utoaji wa chanjo dhidi ya maambukizo ya ungonjwa wa kipindupindu, shughuli amabyo inalenga kuwafikia zaidi ya watu milioni mbili kwenye taifa hilo.

Wilaya 26 ambazo zimeathiriwa pakubwa zinatarajiwa kupewa kipau mbele katika zoezi hilo.
Wilaya 26 ambazo zimeathiriwa pakubwa zinatarajiwa kupewa kipau mbele katika zoezi hilo. AFP
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko wa sasa ambao ulianza mapema mwaka uliopita, umeripotiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 400 wakati wengine zaidi ya 21,000 wakiambukizwa.

Kati ya visa hivyo vya maambukizo, nusu vimeripotiwa kuwaathiri watoto.

Kampeni hiyo inafanyawa kwa ushirikiano wa serikali na mashirika ya Umoja wa Mataifa ambapo raia kati ya umri wa mwaka moja na zaidi wanatarajiwa kuchanjwa.

Wilaya 26 ambazo zimeathiriwa pakubwa zinatarajiwa kupewa kipau mbele katika zoezi hilo.

Taifa hilo la kusini mwa Afrika limekuwa likikabiliwa na mlipuko wa kipindupindu tangu mapema mwaka uliopita.

Zaidi ya watu 188,000 wameambukizwa ugonjwa huo wengine 3,000 wakiripotiwa kufariki katika nchi za  Zimbabwe, Msumbiji na Zambia, kwa mujibu wa shirika la Umoja wa Mataifa Ocha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.